Wananchi wote na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo mnaagizwa kufanya usafi katika mazingira yenu yanayowazunguka sambambsa na kutokutupa taka, kumwaga maji machafu kwenye mitaro au barabarani. Aidha mnaagizwa pia kuchimba mashimo ya kutupia taka kwenye maaeneo yote ya makazi, pamoja na kuweka vyombo maalum kwa ajili ya kuhifadhia taka kwenye maduka na maeneo yote ya biashara. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayekamatwa akichafua mazingira iwe kwa akusudi au kwa bahati mbaya.Tangazo hili limetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Ndg. Agnes Mkandya.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Kichangani, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255232935454
Simu ya Kiganjani: 0754837650
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa