Benki ya Exim tawi la Morogoro imekabidhi madawati 50 yenye thamani ya Shilingi 10 kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe ikiwa ni juhudu za serikali Wilayani Gairo za kuboresha sekta ya elimu na kuongeza ufaulu .
Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabisdhiano hayo yaliyofanyika katika shule ya Msingi Kisitwi, iliyopo kata ya Rubeho, Meneja wa Tawi la Exim Morogoro Bwana Patrick Njole amesema benki yake inatambua umuhimu wa elimu na changamoto zake hivyo madawati hayo yatasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa madawati mashuleni.
“Sisi kama Taasisi inayotoa huduma za Kibenki na Fedha tunaamini kwamba msaada huu wa madawati haya japo ni machache utawawezesha watoto wetu kusoma katika mazingira safi yenye kuvutia na kuamsha ari ya bidii katika kusoma na kujifunza, nah ii inaongeza ufaulu”, alifafanua.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Mchembe akipokea madawati hayo, amemshukuru Menejea huyo na watumishi wote wa Exim Benki kwa kukubali ombi lake la kuchangia zoezi la utengenezaji wa madawati hayo na kwamba mchango huo ni wa thamani kubwa sana katika kuinua ukuaji wa sekta ya elimu wilayani Gairo.
“Kwa kweli nashukuru uongozi mzima wa Exim Benki na watumishi wote kwa kupokea na kukubali ombi langu, niimani yangu kuwa mchango wa madawati utaongeza kasi ya wototo wetu kujifunza na kuongeza ufaulu.
Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya Msingi Kisitwi, wamemshukuru na kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Gairo kwa juhudi zake za kuinua sekta ya elimu, ambapo wamesema watayatunza vyema madawati hayo ili yaweze kutumiwa na vizazi vijavyo.
Exim imetengeneza madawati hayo yakiwa na mchanganyiko wa mbao na vyuma na kuayafanya kuwa imara zaidi ambapo yatadumu kwa muda mrefu ilinganishwa na madawati ya mbao tupu ambayo hulegea na kuharibika kwa muda mfupi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa