WATENDAJI WA VIJIJI, KATA WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA
Na Cosmas Njingo
Watendaji wa Viiji na Kata Wilayani Gairo, wametakiwa kuzingatia sheria na kuchukua hatua kali dhidi wa Wananchi wanaokunywa pombe na kucheza bao muda wa saa za kazi.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kisitwi kilichopo kata ya Rubeho Wilayani Gairo.
“Hii ni hatari sana, Sheria zipo kwa nini Watendaji hamzitumii kuwachukulia hatua hawa wanaolewa muda wa saa za kazi?” alihoji kwa uchungu baada ya kukuta baadhi wa wakazi wa kijiji hicho wakilewa na kucheza bado muda wa saa 7:12 mchana.
Akaendelea “Mtendaji! sijaridhishwa na majibu yako na siwezi kuamini kama ni kweli umeshachukua hatua zozote kwa wale wote ambao wameshindwa kutii agizo la Mkuu wa Nchi Mhe John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amabye amepiga marufuku unywaji wa pombe na kucheza bao muda wa kazi na badala yake watumie muda huo kuzalisha mali.
Mheshimiwa Mchembe alimwagiza mtendaji wa kikijiji hicho kuhakikisha anatumia sheria ndogo zilizopo kuwachukulia hatua wananchi wanaokunywa pombe nyakati za saa za uzalishaji mali, sambamba na kuzingatia malekezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, ya kuwataka wafanya biashara wa huduma za Baa na Klabu za pombe za kienyeji kufungua huduma hizo kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 5:00 usiku.
“Unatakiwa kufuata maelekezo ya mwajiri wako aliyokupatia katika barua yake ya katazo kwa wafanyabiashara wa baa na klabu za pombe za kienyeji inayoagziza kutofanya biashara hizo muda wa saa za kazi, ni lazima ufuatilie kwa ukaribu kama baa na klabu za pombe zinafunguliwa saa 10:00 jioni na kufungwa saa 5:00 usiku.
Akijibu maswali ya Mhe. Mkuu wa Wilaya, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kisitwi Bi Yuster Blazia Omari alisema uongozi wa kijiji kushirikiana na ofisi yake wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali ikiwepo kutoa elimu kwa jamii juu ya maagizo mbalimbali ya viongozi wa juu lakini baadhi ya wnanchi wamekuwa wagumu kutekeleza bila kushurutishwa.
“Mkuu tunajitahidi sana kwalemisha wananchi juu ya jambo hili, lakini changamoto kubwa watu wakishatoka shambani kuanzaia saa 5 hawana kazi nyingine za kufnya ndiyo maana wanakaa baa na vijiweni muda huu”, alibainisha
Mteandaji huyo wa kijiji alifafanua kuwa changamoto kubwa ya wakazi wa vijiji ni asili ya kazi wanazofanya, wengi wao wakiwa ni wakulima ambapo shughuli za kilimo hufanyika nyakati za alfajiri na majira ya saa 6 mchana baada ya hapo hawana shughuli nyingine zaidi ya kilimo.
Mapema hivi Karibuni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa alipiga marufuku uingizaji, usambazaji na uuzwaji wa pombe kali inayohifadhiwa katika vifungashio vya plastiki maarufu kama “VIROBA”.
Upigwaji marufuku wa pombe hiyo umetokana na madhara yanayopatikana baada ya mtumiaji kuitumia ambapo inaelezwa husababisha kuongekeza matukio ya kiuhalifu pamoja na kupunguza uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji mali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa