Na Cosmas Mathias Njingo, GIO Gairo
Maafisa Habari pamoja na Wataalamu wa mifumo ya Kompyuta Serikalini watakiwa kuwafanya kazi kwa kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao ya utoaji taarifa kwa umma, ili kuongeza ufanisi na kuwaweza wananchi kupata taarifa muhimu zenye tija.
Rai hiyo imetolewa Machi 20.2017 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dakta Eng. John Ndunguru, wakati akifungau Warsha ya siku 7 ya mafunzo ya utengenezaji wa tovuti za serikali kwa Maafia TEHAMA na Habari Serikalini.
“Mnapaswa kubadilika, kushirikiana na kufanya kazi kwa bidii, mkitumia vyema taaluma zenu katika kutoa taarifa muhimu kwa Wananchi ili muwezeshe kuondokana na umaskini uliokithiri badala ya kutengana ile hali ninyi ni wamoja”. Alisema.
Dakta Nduguru akabainisha kuwa umefika wakati wa kila mtu kujituma vyema, kuwa mbunifu sambamba na kuangalia mwelekeo wa dunia katika matumizi ya mitandaoya kijamii kwani kwa kufanya hivyo kutarahisisha taarifa zao kuwafikia wananchi kwa haraka na kwa muda mfupi zaidi.
Alisema “zipo njia nyingi sana za utoaji wa taarifa, hasa ikizingatiwa kwamba sasa mwelekeo wa Dunia unazidi kushamiri katika matumizi ya mitandao ya kijamii, hivyo ni vyema mkatumia fursa hiyo ya mitandao ya Kijamii kuwafikia Wananchi”.
Mafunzo hayo ya siku 7 yalianza Machi 20.2017 yakijumuisha washiriki zaidi ya 80 kutoka Halmashauri za Mikoa 5 ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Simiyu na wenyeji Morogoro, yanatarajiwa kukamilika Machi 27.2017, ambapo wataalam hao watakuwa na uwezo wa kutengeneza, kusimamia na kuendesha tovuti za Serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa