Pamoja na baraza nakujadili mambo mbalimbali yahusuyo wilaya pia kulikuwa na matukio makubwa yaliyofanyika kama yafuatayo:
(i)UGAWAJI WA HUNDI KWA AJILI YA MIKOPO KWA VIKUNDI MBALIMBALI VYA WANAWAKE NA VIJANA.
Mhe. Mwenyekiti alimkaribisha Mhe. Mbunge Ahamed Shabiby kukabidhi hudhi kwa vikundi mbalimbali vilivyoomba mikopo kama ifuatavyo;
Na | JINA LA KIKUNDI | MAHALI | SHUGHURI ZA KIKUNDI | KIASI KILICHO KOPESHWA |
1 | Chapakazi | Kibedya | Ufugaji wa Mbuzi | 1,500,000.00 |
2 | Songambele
|
Rubeho | Ufugaji wa Nguruwe
|
1,000,000.00 |
3 | Agape | Chigela | Uzalishaji wa viazi lishe | 1,000,000.00 |
4 | Maisha kujitegemea | Ng'olongo-Idibo | Ufugaji wa Mbuzi
|
1,000,000.00 |
5 | Mnangalini | Magoweko | Saluni | 2,000,000.00 |
6 | Kazi kwanza | Kibedya | Ufugaji wa mbuzi
|
1,000,000.00 |
7 | Neima IR VIKOBA |
|
|
3,000,000.00 |
8 | Tumaini |
|
|
1,000,000.00 |
9 | Chikikole B | Italagwe | Ufugaji wa mbuzi
|
1,5000,000.00 |
|
JUMLA |
|
JUMLA |
13,500,000.00/= |
Mhe Mbunge aliwasihi wanavikundi wote waliokopeshwa kuzitumia vizuri fedha hizo ili ziwasaidie kujikwamua kiuchumi na vilevile waweze kuzirejesha.
Marejesho ya mkopo kwa kikundi kilichokuwa kimekopeshwa na Halmashauri.
Kikundi cha Nyota ya matumaini kilichopo kijiji cha Chakwale kilifanikiwa kurejesha fedha kiasi cha Tshs 1,100,000 kutoka kiasi cha Tshs 1,000,000.00 ambazo walikopeshwa na Halmashauri. Aidha wanakikundi waliishukuru Halmashauri kwa namna inavyosaidia wananchi wake kujikomboa kiuchumi kwa kuwapa mikopo.
(ii) Motisha kwa Walimu saba wa Shule ya Sekondari Gairo waliofaulisha vizuri masomo yao katika mtihani wa kidato cha sita 2017 walizawadiwa kama ifuatavyo:
Na | JINA | SOMO AU CHEO | ZAWADI |
1 | Mwl. Jones Nyato | Mkuu wa Shule | Cheti |
2 | Ally Sheria | Historia | 100,000 .00 na cheti |
3 | Boniface Mluba | Biolojia | 100,000.00 na cheti |
4 | Hamisi Maneno | Kingereza | Cheti |
5 | Damaris Kapere | Kingereza | Cheti
|
6 | Nassoro M. Wanogile | Historia | Cheti
|
7 | Rajab mgonja | Jiografia | Cheti
|
Mhe Mbunge Ahamed Shabiby aliwasihi walimu hao kushirikiana na walimu wengine ili kuongeza bidii Zaidi katika kuinua ufaulu kwa wanafunzi aidha aliahidi kutoa zawadi ya TShs 100,000 kwa kila mwalimu aliyefaulisha vizuri somo lake katika Mtihani wa kidato cha sita 2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa