Katika kikao hiki cha baraza maalum la ushauri Viongozi wa taasisi mbalimbali waliwasilisha taarifa za utendaji kazi kama ifuatavyo:
Alisema SIDO inatengeneza mashine za aina mbalimbali kwa ajili ya shughuli za ujasiliamali. Alishauri jamii kushirikiana na SIDO katika kujiinua kiuchumi.
Wajumbe walitoa hoja kuwa ni vema wafanyabiashara kupitia TCCIA wakashirikiana na SIDO katika kuwainua kiuchumi wajasiliamali wa Gairo.
Mwakilishi kutoka Shirika la Nyumba aliwaeleza wajumbe kuwa lengo la shirika hilo ni kuwasaidia wananchi kwa kujenga nyumba za kupangisha kwa bei nafuu au kujenga nyumba za aina mbalimbali na kuziuza.
Alifafanua kuwa mawasiliano yanafanyika ili kuona namna NHC itakavyotekeleza miradi hiyo katika Wilaya ya Gairo.
Meneja wa TANESCO (W) aliwaeleza wajumbe kuwa katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa umeme, TANESCO inafanya utaratibu wa kuunganisha umeme kutoka Wilaya ya Mpwapwa - Dodoma na Mtibwa Wilayani Mvomero - Morogoro ili inapotekea umeme wa Wilaya Moja umekatika Gairo iweze kutumia umeme wa Wilaya nyingine.
Alizitaja shughuli mbalimbali zilizotekelezwa na TANESCO kama vile kuendelea na usambazaji wa nguzo za umeme kwa wananchi pamoja, kutoa elimu juu ya matumizi bora ya umeme pamoja na kufanya ufuatiliaji kwa wote wanaovunja sheria za matumizi ya umeme.
Baada ya taarifa kuwasilishwa, wajumbe walitoa hoja zifuatazo:
Meneja wa Benki ya NMB aliwaeleza wajumbe kuwa, Benki ya NMB inatoa huduma mbalimbali kwa ajili ya kuwakomboa wananchi kiuchumi. Aliwaasa wananchi kuchangamkia fursa zinazotolewa na NMB ikiwa ni pamoja na mikopo ya aina mbalimbali kwa ajili ya kuwakomboa wananchi kiuchumi.
Wajumbe walitaka kufahamu ni sababu gani inayosababisha kuchelewa kutolewa kwa mikopo mara mteja anapokamilisha taratibu zote za maombi ya mkopo.
Ilielezwa kuwa kwa kawaida mkopo hutoka ndani ya wiki mbili tangu mteja alipokamilisha taratibu zote za maombi ya mkopo. Aidha ikiwa kuna tatizo mteja atajulishwa kwa ajili ya kufanya marekebisho.
Meneja wa benki ya CRDB aliwashauri wajumbe kutumia fursa za mikopo inayotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi. Alieleza kuwa CRDB inatoa mikopo ya aina mbalimbali kama vile, pikipiki, bajaji, vikoba, biashara na mikopo kwa watumishi.
Wajumbe walitaka kufahamu ni namna gani Benki inavyoweza kuwasidia wafanyabiashara waliokopa na biashara zao kuyumba na kusababisha kushindwa kurejesha mkopo kwa wakati na utaratibu uliokubaliwa.
Ilielezwa kuwa mawasiliano hufanyika kati ya Mteja na Benki ili kufanya makubaliano kwa ajili ya urejeshaji mikopo kwa wafanyabiashara walioyumba kibiashara.
Meneja wa TARURA aliwaeleza wajumbe kuwa TARURA Gairo inaendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za ujenzi wa miundo mbinu ya barabara kwa ubora unaokubalika. Alifafanua kuwa katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2018/2019 TARURA imeomba kiasi cha TShs. Bilioni 10 kwa ajili ya matengenezo ya barabara zenye urefu wa Km.621.63 za Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa