KUKAMILIKA KWA UJENZI WA ZAHANATI YA KISITWI KWALETA TUMAINI JIPYA KWA WANANCHI.
Na Cosmas Njingo
Ushiriki wa wananchi katika kubuni, kuibua na kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii ikiwepo ujenzi wa zahanati na vituo vya kutolea huduma za afya ni kati ya nguzo za kuinua diplomasia ya kujiletea maendeleo yao kwa kupambana kivitendo vita dhidi ya maradhi, ujinga na Umasikini.
Kupitia Serikali ya awamu ya tano ya Dakta John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia ikiongozwa na dhana ya uwajibikaji chini ya falsafa ya ‘HAPA KAZI TU’, Wananchi wengi hususani waishio vijijini wamepatwa na msukumo mkubwa katka kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kukuza ustawi wa mustakabali wa maisha yao.
Jamii imeweza kuibua miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi katika maeneo yao, hali ambayo inadhihirisha kufanikiwa kwa Falsa ya Mhe. Rais Magufuli ya “Hapa kazi tu”.
Hivi karibuni nilifanya ziara ndogo katika kijiji cha Kisitwi, kilichopo kata ya Rubeho Wilayani Gairo, ambapo ziara yangu ilivutiwa sana na mwamko wa jamii ya kijiji hicho namna ambavyo imepania kuhakikisha inaimarisha upatikanaji wa huduma za afya kijijini hapo kwa kuibua mradi wenye thamani ya shilingi za Kitanzania 49,176,000 wa ujenzi wa jengo la zahanati ya kijiji.
Kukamilika kwa Mradi huu wa uboreshaji huduma za afya katika kijiji cha kisitwi kutasaidia kupunguza vifo vya wanawake wajawazito pamoja na watoto wachanga ambao walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata, huduma za afya kwenye makao makuu ya kata.
Mtendaji wa Kata ya Rubeho, Salum Dibega anaeleza kuwa mradi huu uliibuliwa na wananchi wenyewe na kuanza kutekelezwa mwaka 2006.
“Ni wananchi wenyewe walikaa na kuamua kuibua mradi wa ujenzi wa zahanati, hii ni baada ya kukukabiliana na changamoto ya upatikanai wa wahuduma za afya jirani na makazi yao” alifafanua na kuengele,
“Kimsingi utaona tangua mwaka 2006 ni miaka 10 imepita, lakini chanamoto kubwa ilikuwa ni mwamko mdogo katika kuchangia nguvu kazi na rasilimali fedha, lakini baada ya kushirikishwa kikamilifu wakaelewa umuhimu wa mradi huu kwa kweli saizi mambo ni mazuri”, alelezea.
Mtendaji huyo akataja kuwa Mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo unatarajiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma za afya mwezi Aprili mwaka huu. Ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuendelea kuchangia nguvu kazi na fedha kwa ajili ya kuharakisha umaliziaji.
Jenego la Zahanati ya Kisitwi linakadiriwa litagharimu kiasi cha Shilingi 49,176,000 hadi kukamilika ambapo hadi sasa jumla ya shilingi 36,611,500 zimeshatumika na kwamba kiasi hicho cha fedha kimetokana na vyanzo mbalimbali ikiwepo michango ya Wananchi shilingi 9,200,000 na wadau wengine wamechangia shilingi 750,900 kupitia harambee.
“Pia tunamshukuru Mhe. Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe. Shabiby kwa kujiolea mifuko 50 ya saruji yenye thamani ya shilingi 7,500,000 pamoja na Serikali kupita Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kutuwezesha kwa kiasi cha fedha cha shilingi 19,376,500”, alichanganua Mtendaji huyo.
Kisitwi wamethubutu na wameweza…Je wewe? Huu uwe ni mfano wa kuigwa, jamii nzima itambue umuhimu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili kutekeleza kwa vitendo Falsafa ya “HAPA KAZI TU”
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa