MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhe. Rachel Nyangasi, amewaagiza waheshimiwa madiwani Wilayani humo kuelimisha na kuhamasisha jamii itumie chakula kilichopo vizuri, sambamba na kuweka hakiba ili kuepukana na upungufu wa chakula.
Ametoa agizo hilo wakati akifungua kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kilichofanyika Aprili 6 2017 kujadili taarifa za utekelezaji kwa kipindi cha robo ya pili kuanzia Mwezi Oktoba 2016 hadi Desembe 2017.
“Nawaagiza Wahe. Madiwani, mkahakikishe mnahamasisha wananchi katia kata zenu watumie vizuri chakula walichonacho, na kuwaelimisha juu ha umuhimu wa kuweka hakiba ili tuondokana na malalamiko ya upungufu wa chakula”
Kwa upande mwingine amewataka Wahe.Madiwani hao waendelee kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kijami ikiwa ni pamoja na kuchangia shughuli za maendeleo hususani uchangiaji wa matofali kwa ajili ya kuwa na benki ya kutosha ya matofali.
“Wananchi wahamasishwe waendelee kushiriki uchangiaji wa tofali ili kila kijiji na kila kata kuwe na Benki ya tofali zakutosha kwa jili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa majengo ya kijamii kama zahanati na shule.
Hata hivyo Mhe. Nyangasi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Chigela aliwashauri wajumbe wa Baraza lake kuwa ni vyema kusimamia utekelezaji wa miradi ya kijamii ili fedha zinazotolewa na Serikali katika kutekeleza miradi hiyo iwe na tahamani sawa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe.Siriel Shaidi Mchembe aliwataka Wahe. Madiwani hao kutokutumia kama ofisi za watendaji wa vijiji na kata, majengo yaliyojengwa kwa matumizi ya maghara ya kuhifadhia chakula kwenye maeneo yao na kuwaagiza wahakikishe ofisi hizo zihamishwe haraka katika maghara hayo.
“Mhe. Mwenyekiti nakushukuru kwa kutoa angalizo kwa wananchi kuhifadhi chakula, nami naomba nitoe agizo kwakmba ofisi za watendaji zilizopo kwenye majengo ya maghara ya vijiji na kata zihamishwe haraka ndani ya kipindi cha miezi 6 kuanzia sasa”, alisisitiza Mhe. Mchembe.
Aidha akizungumzia swala la mimba za utotoni hasa kwa Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari Wilayani Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya Wahe.Madiwani na watendaji wa serikali kuwafumbia macho watuhumiwa wa kuwapa mimba wananfunzi huku akisisitiza kuwa yeyote atakayebainika kushiriki kumaliza kesi za mimba nyuma ya pazia hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa