Mkutano huo ulikuwa maalumu kwa ajili ya Kujibu hoja za ukaguzi, Katibu alimkaribisha Mwenyekiti kufungua Mkutano, akifungua mkutano huo Mwenyekiti aliwakaribisha wajumbe pamoja na kumweleza Mkuu wa mkoa kuwa hoja zilizopo sio nyingi kwa kuwa tumejitahidi sana kupunguza hoja kwa kufanya kazi kwa weledi hivyo hoja zilizopo ni chache na nyingine nyingi tumeshazijibu na ziko tayari kwaajili ya kwenda kukaguliwa.
Mwenyekiti alimwomba Mkuu wa mkoa kuwahimiza Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kuwalipa madeni yao ili kufanikisha maagizo mengine kutoka LACC ambayo yanawafanya wao kama halmashauri kutokuwa na majibu kwa kuwa madeni hayo hayajalipwa .
Pia mwenyekiti alimweleza Mkuu wa Mkoa na wajumbe wengine kuwa Changamoto ya Uhaba wa Mapato katika halmashauri ya Gairo pia ni chanzo mojawapo cha kushindwa kujibu hoja hivyo tunajitajidi kubuni vyanzo mbalimbali ili kuongeza Mapato na uhaba wa Wakaguzi wa ndani pia ulisababisha Halmashauri kutokufanya vizuri.
Naye Mkuu wa Morogoro Mh.kebwe Steven Kebwe amepongeza Halmashauri kwa Kufanya Mkutano huo wakati wa karibia nakufunga mwaka wa Srikali kwa Kuwa tutakapoanza tutakuwa wapya, huku akihimiza kutekelezwa kwa auli mbiu za mheshimiwa Rais za kupambana na mafisadi, kuombea amani ya nchi, rushwa, uwajibikaji katika utendaji kazi yaani nidhamu kwa watumishi wa umma na kutekeleza kauli mbiu ya “hapa kazi tu”.
Pia mkuu wa Mkoa aliupongeza Mkoa wa Morogoro kwa kutokupata hati ya mashaka na kusisitiza kuwa sasa tusilewe na hizo sifa kwa kufanya kazi kwa weledi na na kwa heshima hiyo Mkoa umepewakipaumbele cha ufundishaji wa masuala ya mifumo ya udhibiti wa masuala mazima ya kifedha ili tuweze kuboresha zaidi na mikoa mingine watakuja kujifunza kwetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa