SERIKALI YA CHINA KUINUA SEKTA YA KILIMO NA VIWANDA VIDOGO TANZANIA
SERIKALI ya China imesema itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania katika kuimarisha uchumi kwa kuwezesha sekta za Viwanda, Kilimo na Mifugo endelevu kwa lengo la kutekeleza diplomasia ya mapinduzi ya kiuchumi kwa vitendo.
Hayo yamebanika Machi 28 2017 Jijini Dar es salaam wakati wa mazungumzo kati ya Balozi wa China Nchini Tanzania Dkt. LU Youging na Msaidizi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya maswala ya Wanawake, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo .
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za Ubalozi China Nchini ambapo pamoja na mambo mengine, Balozi Youging alisema China inatambua vyema ushirikiano ulipo kati ya serikali yake na Serikali ya Tanzania.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Mchembe katika mazungumzo baina yake na Balozi LU Yougin, Serikali ya China inaelenga kusaidia katika kukifanya kilimo cha Tanzania kuwa cha kisasa chenye matokeo chanya kwa wakulima ili kukifanya kiwe kilimo cha kibiashara zaidi kwa kutumia teknolojia za kisasa katika uzalishaji.
“Leo tarehe 28 March 2017, nimefanya mazungumzo na Balozi wa China Nchini Tanzania, kwa kweli mazungumzo yetu yamekuwa na tija kubwa sana kwani tunatarajia kuona mabadiliko katika sekta ya kilimo, ambapo Serikali ya China itasaidia kukifanya kilimo chetu kiwe cha kibiashara zaidi”, alibainisha Mkuu huyo wa Wilaya.
Mbalina na Sekta ya Kilimo, uimarishaji wa Viwanda vidogo kwa ajili ya vikundi wa wanawake wajasiriamali kupitia shughuli za uzalishaji na usindikaji wa mafuta ya alizeti nalo likapewa chumba atika mazungumzo hayo sambamba na kujadili juu ya Mkakati wa ujenzi wa Soko la Kisasa la Mahindi na Maghara ya kuhifadhia chakula Wilayani Gairo.
Aidha Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Siriel Mchembe ameshukuru na kuipongeza Serikali ya China kwa namna inavyoshiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo hasa kwa kuonyesha nia ya kuwezesha vikundi vya wanawake kujikwamua kiuchumi na kujiendeleza kimitaji kupitia huduma za viwanda vidogo na kwamba amemualika Balozi Lu kuja Gairo ili kujionea fursa mbali mbali zilizopo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa