Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mh. JOSEPH KAKUNDA(MB) akizungumza na Watumshi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo alipofanya ziara ya kutembelea Miradi ya Elimu mnamo tarehe 2/10/2018.
Waziri Kakunda alisisitiza kuwa ni jukumu la kila Mtumishi wa Halmashauri kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha utekelezaji wa Miradi mbalimbali iliyoanzishwa na itakayoanzishwa inasimamiwa ili iweze kukamilika kwa wakati hasa Mradi wa maji ufuatiliwe kwa ukaribu ili uweze kupunguza kero ya maji Gairo.
Alisisitiza kwakuwa miradi ya elimu aliyoitembelea ikamilike mapema na alitoa ushauri kuwa Halmashauri ibuni vyanzo tofauti tofauti vya Mapato ili kuboresha makusanyo yake ya ndani na kuweza kusaidia Miradi ya Maendeleo na pia aliongeza kwa kusema Miradi ya kimkakati iwekewe umakini ili kuongeza mapato na Halmashauri ihakikishe inafuatilia wananchi waweze kulipa kodi.
Mh.Kakunda aliongeza kusema Mh.Rais John Pombe Magufuli anaipenda nchi hii na anania ya kuisaidia Tanzania na ndio maana anahakikisha Miradi ya Msingi ambayo haikukamilika inakamilishwa, pia anahakikisha afya za watanzania zinakuwa njema kwa kujenga vituo vya afya ikiwemo na kutoa pesa za ukarabati wa Kituo cha Afya Gairo. Aliongeza kwa kusema sekta ambayo Mh.Rais kaipendelea ni elimu ili kwa kuwa anapenda waondokane na adui Ujinga.
Mwisho Naibu Waziri Kakunda alisisitiza suala la mahusiano katika kazi alisema " mahusiano yapo katika Dhima sio Dira" hivyo ni lazima na huwa hayaombwi, hivyo ni lazima kuwe na mgawanyo wa kazi na watumishi waheshimiane katika ngazi za Utumishi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa