Huduma za Usajili wa Leseni za Biashara
A. Mahitaji Muhimu wakati kupata Leseni mpya ya Biashara.
1. Fomu ya Maombi (Inapatikana Ofisi ya Biashara Wilaya)
2. Jina la/Majina ya Baishara (yataonekana kwenye leseni yako).
3. Kama ni kampuni aje na nakala ya cheti ya usajili wa BRELA (Certificate of Registration)
4. Nakala ya cheti cha namba ya utambulisho wa mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA (TIN NUMBER).
5. Cheti Orijino cha kuonyesha hudaiwi kodi (Tax Clearance Certificate) kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
6. Ada ya Maombi Tsh.1, 000/-
7. Ada za leseni kwa Mwaka (zinatofautina kulingana na aina ya baishara)
Kwa usajili wa biashara za zilizopo chini ya Mamlaka nyingine Mfano Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), biashara hizo ni kama vile Maduaka ya Dawa za Binadamu, Vinywaji laini, Maduka ya Pembejeo za Kilimo na Mifugo pamoja na maduka ya vyakula mnatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatavyo:-
(a). Cheti cha Cha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) au Mamlaka nyingine
(b) Cheti cha Vipimo vya Afya
(c) Pamoja na viambatanishi vingine vilivyotajwa hapo juu.
B. Kwa wafanyabiashara ambao leseni zimeisha muda wake/wanaohuisha (renew), wanatakiwa kuja na:-
1. Nakala ya leseni ya zamani (Iliyoisha muda wake)
2. Cheti orijina cha kuonyesha hudaiwi kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzani-TRA (Tax Clearance Certificate)
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Afisa Biashara Wilaya ya Gairo kwa simu namba:
0714 067774
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa