Wahemiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji, wakati wa mafunzo kwa Wah. Madiwani kuhusu Madhara ya SUMUKUVU na udhibiti wa athari zitokanozo na Sumu katika mazao ya Karanga na Mahindi.
Mafunzo yaho ya siku moja, yanayotekelezwa chini ya Mradi wa TANIPAC yamefanyika machi 6.2023, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
Mradi wa TANPAC umefanikisha kutekeleza ujenzi wa Ghala kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi tani 1,500 za mazao, ambapo umegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja katika katika kijiji cha Kimashale kata Chakwale unatarajiwa kuleta tija kubwa kwa wakulima wa zao la Mahindi na Karanga ambayo yanatajwa kuwa mazao pekee yanayoathiriwa na kuvu kwa kiwango kikubwa.
Ujenzi huo umehusisha majengo manne likiwepo Jengo la Ghala, Maabara na Kibanda cha Mlinzi na Ofisi ya Watalaam na watumishi wengine.
Miundimbinu mingine ni sehemu ya kuanikia mazao, Kihenge cha kuhifadhia taka, tangi la maji la ujazo wa lita 20,000 na vifaa vya tahadhari kama ving'ora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa