• Mawasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
GAIRO DISTRICT COUNCIL
GAIRO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Authorities Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira
    • Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni za Halmashauri
      • Seksheni ya Rasilimali Watu
      • Seksheni ya Utawala
    • Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Baraza la Madiwani
  • Miradi
    • Miradi ya Maendeleo
      • Sekta ya Elimu Msingi
        • Miradi Mipya
        • Miradi iliyokamilika
      • Sekta ya Elimu Sekondari
      • Sekta ya Afya
      • Sekta ya Barabara/Miundombinu
      • Sekta ya Maji
  • Machapisho
    • Katiba ya JMT
    • Sheria ndogo ndogo za Halmashauri
    • Hotuba Mbalimbali
    • Sera ya Elimu
    • Taarifa za Hesabu za Mwisho
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA, AJALI, AFYA YA AKILI YANAZUILIKA

Posted on: November 10th, 2022

Na. WAF - Mwanza 

Imeelezwa kuwa mbinu muhimu za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na kubadili mtindo wa maisha kwa kudhibiti matumizi ya vilevi kama sigara na pombe, matumizi ya sukari na chumvi, kufanya mazoezi ya mwili pamoja na kuepuka tabia bwete.

Akifungua Kongamano la nne la Kisayansi katika wiki ya maadhimisho ya wiki ya Magonjwa Yasiuoambukiza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.

James Mdoe amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu na kununua vifaa tiba vya kisasa vikiwemo vifaa vya uchunguzi vinavyowezesha wanasayansi kufanya kazi zao kiurahisi ili kugundua magonjwa mapema hususan yasiyoambukiza.

"Kwa sasa tumeshuhudia maboresho yaliyofanyika katika taasisi zetu za Ocean Road, NIMR, JKCI, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali za Kanda, Hospitali za Mikoa, Wilaya hadi Zahanati pamoja na Hospitali binafsi." Amesema Prof. Mdoe

Huduma za Uchunguzi na utambuzi wa magonjwa (Maabara), Mionzi na Radiolojia zimeboreshwa kwa maana ya miundombinu na vifaa vya kisasa ili kurahisisha utoaji huduma ya magonjwa yasiyoambukiza na uwezo wa kufanya tafiti mbambali za kisayansi.

Aidha, Prof. Mdoe ametoa wito kwa taasisi kujiwekeza katika kutoa huduma, waongeze kasi pia ya kufanya tafiti za kisayansi zitakazowezesha wananchi kujikinga na magonjwa haya na pia zitakazowezesha kutoa mbinu mpya za matibabu

Pia, amewataka wataalamu hao kujadiliana juu ya matumizi ya dawa za asili ambazo nyingine zimekuwa zikitumika kutibu pumu, shinikizo la juu la damu na Saratani.

"Tuweke mfumo sahihi wa kuwezesha dawa hizi za asili zikithibitika kisayansi kuwa zinatibu na hazina madhara ili tuweze kuzitumia kudhibiti magonjwa haya yasiyoambukiza." Amesema Prof. Mdoe

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan inaendelea kufanya kazi na wadau wote wenye nia ya kusaidia mapambano dhidi ya magonjwa Yasiyoambukiza, kwani bila kufanya hivyo mlipuko wa magonjwa haya utaendelea kuua watu wengi, kuleta ulemavu na mwisho kurudisha nyuma jitihada za Taifa kukuza uchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za Tiba Prof. Paschal Ruggajo amempongeza Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kulipa kipaumbele swala la mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza na sasa ameipa kazi Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi, kifua kikuu kusimamia maswala ya Magonjwa Yasiyoambukiza.

"Tunatambua mchango mkubwa wa Bunge katika kuimarisha afya za watanzania." Amesema Prof. Ruggajo.

Wizara ya Afya kupitia Idara ya Huduma za Tiba inaratibu kitengo na Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza, inatekeleza afua mbalimbali ili kuongeza nguvu na kuweza kufikia malengo ya kuzuia na kudhibiti Magonjwa hayo.

"Hii kauli mbiu ya mwaka huu ya Badili Mtindo wa Maisha, Boresha Afya lengo lake kuu ni kuitaka jamii ya watanzania na wadau wote kushirikiana katika kubadili mtindo wa maisha ili kuwa na afya bora na yenye kuleta tija kwa Taifa letu." Amesema Prof. Ruggajo

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUITWA KWEYE USAILI WAOMBAJI NAFASI ZA AJIRA MTENDAJI WA KIJIJI III NA DEREVA II September 21, 2024
  • TANGAZO LA HALMASHAURI KUKUSANYA USHURU WA USAFI May 07, 2024
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA PROGRAM YA BBT May 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA DEREVA July 12, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAJALIWA AFUNGUA TAWI LA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR MKOA WA MOROGORO

    July 17, 2024
  • GAIRO SEKONDARI YATEKELEZA AGIZO LA KULIMA BUSTANI ZA MBOGAMBOGA, MATUNDA

    July 15, 2024
  • MARUFUKU KUUZA, KUNUNUA MAZAO KWA KUPIMA KWENYE NDOO, MADEBE

    July 12, 2024
  • KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI

    July 11, 2024
  • Tazama zote

Video

WANAFUNZI DARASA LA SABA WAASWA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni za Manunuzi
  • Zabuni za Ujenzi
  • Huduma

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Tanzania
  • GAIRO ONLINE TV
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Mawasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.

    Sanduku la Posta: 40, GAIRO

    Simu ya Mezani: +255 787730665

    Simu ya Kiganjani: +255 717222572

    Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa