Na, Cosmas Njingo. GAIRO
23.04.2024
Mradi wa upanuzi wa miundombinu ya maji Makuyu kwenda Kinyolisi na Iyogwe ni mradi uliotekelezwa kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Mkataba wa mradi huu ulisainiwa tarehe 07 Januari, 2022 baina ya Mkandarasi M/S SIBIKA TRADERS and CONSTRUCTION LIMITED wa Dar Es salaam na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Morogoro ambapo utekelezaji wake ulianza rasmi tarehe 17 Januari, 2022 na kukamilika tarehe 16/07/2022.
Kutokana na changamoto ya mvua kuathiri upelekaji wa vifaa eneo la mradi na Mkandarasi kuwa kwenye mchakato wa kuomba kusamehewa kodi. Miradi huu umewekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa tarehe 22 Agosti, 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa