Na. Cosmas Mathias Njingo
Kutoka:wizara_sanaatz. Agosti 6.2022
Waziri wa Utamaduni, Sanaa Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana na ujumbe wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na ameunda tume kwa ajili ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiswahili nchini ikiwa ni mkakati kabambe wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili katika mabara yote duniani.
Mhe, Mchengerwa ameunda tume maalum ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Kiswahili kufuatia ombi lake alilolitoa kwa shirika la UNESCO wakati wa siku ya maadhimisho ya Kiswahili duniani mwaka huu iliyofanyika kwa mara ya kwanza Julai 7, 2022.
Akizungumza mara baada ya mkutano na ujumbe wa UNESCO ofisi za Tanzania leo Agosti 5, 2022 ofisini kwake jijini Dar es Salaam amesema matajio ya Serikali ni kuona kuwa Kiswahili kinavuka mipaka ya Tanzania.
Aidha, Mhe Mchengerwa ameipa tume hiyo siku tano kukamilisha andiko hilo ili liwasilishwe kwenye ngazi za juu kwa ajili ya maamuzi.
Amesema hadi sasa tayari Serikali imetenga na kutoa ekari mia moja kwa ajili ya kujenga chuo hicho ambacho kinatarajiwa kuwa kitalu cha kuzalisha, kuhifadhi na kuendeleza lugha adhimu ya Kiswahili kwenye mataifa mbalimbali duniani.
Amesema katika kikao hicho pamoja na mambo mengine pia wamejadili namna ambavyo wanaweza kuendeleza na kukuza Kiswahili na kuwa nyenzo ya kufundisha lugha ya Kiswahili kwenye lugha nyingine kubwa zakimataifa.
Amefafanua kuwa uanzishwaji wa chuo kama hiki ni jambo ambalo limeshafanyika kwenye mataifa mengine duniani na kuleta mafanikio makubwa hivyo hakuna sababu ya Tanzania kisiwepo, sehemu ambayo ndiyo chimbuko na kiini cha Kiswahili duniani
Amesema namna bora ya kubidhaisha Kiswahili ni kuwa na chuo maalum ambacho kitajikita kwwnye kuendeleza lugha ya Kiswahili na lugha ndogondogo ambazo zimekuwa zikisaidia katika kutoa misamiati kadhaa ya Kiswahili.
Aidha, amesisitiza kuwa chuo hicho kitasaidia kuhifadhi lugha nyingine ndogondogo ambazo zinakwenda kufa ambapo pia kitasaidia kufanya utafiti wa kina kwenye eneo la Kiswahili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa