October 10. 2022
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele katika kuhakikisha wanawake na watoto wa kike wanapata huduma wezeshi zikiwemo za afya na elimu ili kuwezesha kujenga jamii yenye usawa.
Ameyasema hayo alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Viongozi wa Ngazi za juu ya kuwezesha Viongozi Wakuu kuhusu kuwezesha Vipaumbele vya Wanawake na Wasichana katika Mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi uliofanyika Oktoba 10, 2022 Serena Hoteli jijini Dar Es Salaam.
“Wasichana wakipata elimu bora wataweza kuepukana na maambukizi ya virsri vya ukimwi, kuanzia katika ngazi ya familia na jamii kwa ujumla, hivyo ni wajibu wetu kuwekeza kwa watoto wa kike ili kuwa na jamii yenye mafanikio na usawa katika maendeleo.” Alisema Mhe. Majaliwa.
Amesema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha wanaweka kipaumbele katika kuwahudumia wanawake wanaoishi na VVU ikiwemo kuviwezesha vikundi vyao, kutoa elimu pamoja na kuwajumuisha katika ngazi za maamuzi kwenye sehemu za kutolea huduma za afya.
Waziri Mkuu amesema katika kufanikisha mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi ni vyema watoto wa kike wakapewa nafasi katika utungaji wa Sera na miongozo ya kupambana na ugonjwa huo itaongeza ufanisi katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo kwani kundi hilo limekuwa sehemu ya waathirika wakubwa.
Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe. @Ummymwalimu amempongeza Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa kwa kuwa kuwa kinara katika kuongoza mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi.
Waziri Ummy amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake (UN WOMEN) Serikali ya Marekani kupitia PEPFAR pamoja na Global Fund pamoja na wadau wengine kwa kuwezesha utekelezaji wa afua za mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi pamoja na Kifua Kikuu.
Waziri Ummy amesema kuwa kupitia kikao hicho nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara zitaweka mikakati ya pamoja ili kusonga mbele katika kumkomboa mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla pamoja kuweka mikakati ya kuwalinda dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa