• Mawasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
GAIRO DISTRICT COUNCIL
GAIRO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Authorities Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira
    • Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni za Halmashauri
      • Seksheni ya Rasilimali Watu
      • Seksheni ya Utawala
    • Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Baraza la Madiwani
  • Miradi
    • Miradi ya Maendeleo
      • Sekta ya Elimu Msingi
        • Miradi Mipya
        • Miradi iliyokamilika
      • Sekta ya Elimu Sekondari
      • Sekta ya Afya
      • Sekta ya Barabara/Miundombinu
      • Sekta ya Maji
  • Machapisho
    • Katiba ya JMT
    • Sheria ndogo ndogo za Halmashauri
    • Hotuba Mbalimbali
    • Sera ya Elimu
    • Taarifa za Hesabu za Mwisho
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

UVCCM WILAYA YA GAIRO WAPONGEZWA KWA HAMASA KUBWA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2024

Posted on: April 26th, 2024

COSMAS MATHIAS NJINGO. GAIRO

APRILI 26. 2024

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava, amewapongeza Vijana wa hamasa wa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya a Gairo kwa kazi kubwa ya kukimbiza mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2024.

Ametoa pongezi hizo ApriIi 22. 2024 alipokuwa akiaga uongozi na Wananachi wa Wilaya ya Gairo tayari kwa safari kuelekea Wilaya ya Kilosa, mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuhitimisha mbio zake Wilayani Gairo Aprili 21.2024.

“Ninapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Vijana wenzangu wa hamasa kwa kazi kubwa na nzuri ya kukimbiza mwenge wa Uhuru. Hakika Vijana wa Hamasa wamekuwa na Hamasa kubwa sana ya kizalendo ya kushiriki mbio za Mwenge wa Uhuru. Lakini pia nikupongeze Mhe. Mkuu wa Wilaya na Uongozi Mzima wa Halmashauri kwa maandalizi mazuri ya kuupokea na kukimbiza Mwenge wetu wa Uhuru.

Mnzava alisema Mbio za Mwenge wa Uhuru zinawakilisha Itifaki ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuongeza kuwa mwenge unapaswa kukimbizwa na siyo kutembezwa huku akifurahishwa na kuona Wananchi walijitokeza kwa wingi kuupokea mwenge wa Uhuru katika Miradi yote ya maendeleo iliyofikiwa na Mwenge huo.

“Kwa kweli niseme kuwa Wananchi wa Wilaya ya Gairo, wametendea haki mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu kwani tumekutana na hamasa kubwa kwenye miradi yote Wananchi walijitokeza kwa wingi na tumeona hamasa kubwa imefanyika. Nawapongeza sana Viongozi wote wa Wilaya ya Gairo chini ya Mhe. Mkuu wa Wilaya, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Ofisi ya Mkurugenzi kwa maandalizi mazuri.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame amewashukuru Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wote, kwa ushirikiano Mkubwa waliouonesha kipindi chote cha kukimbiza Mwenge ambao ulipita katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kujionea shughuli za utekelezaji wa miradi hiyo, kuweka mawe ya msingi, kuzindua na kufungua ili Wananchi wapate huduma.

“Nami kwa niaba ya Viongozi wenzangu pamoja na Wananchi wa Wilaya hii ya Gairo, nipende kukushukuru Wewe Ndugu yangu Comredi Godfrey Mnzava na Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wenzano Kitaifa kwa kutupa ushirikiano mkubwa wakati wa shughuli za Mbio wa Mwenge wa Uhuru.

Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 inasema “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUITWA KWEYE USAILI WAOMBAJI NAFASI ZA AJIRA MTENDAJI WA KIJIJI III NA DEREVA II September 21, 2024
  • TANGAZO LA HALMASHAURI KUKUSANYA USHURU WA USAFI May 07, 2024
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA PROGRAM YA BBT May 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA DEREVA July 12, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAJALIWA AFUNGUA TAWI LA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR MKOA WA MOROGORO

    July 17, 2024
  • GAIRO SEKONDARI YATEKELEZA AGIZO LA KULIMA BUSTANI ZA MBOGAMBOGA, MATUNDA

    July 15, 2024
  • MARUFUKU KUUZA, KUNUNUA MAZAO KWA KUPIMA KWENYE NDOO, MADEBE

    July 12, 2024
  • KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI

    July 11, 2024
  • Tazama zote

Video

WANAFUNZI DARASA LA SABA WAASWA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni za Manunuzi
  • Zabuni za Ujenzi
  • Huduma

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Tanzania
  • GAIRO ONLINE TV
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Mawasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.

    Sanduku la Posta: 40, GAIRO

    Simu ya Mezani: +255 787730665

    Simu ya Kiganjani: +255 717222572

    Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa