Na. Cosmas Mathias Njingo. 88 MOROGORO
Agost 8.2023.Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Waziri Kindamba amewataka wakulima kulima Kilimo Baashara, sambamba na kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ili kukidhi mahitaji ya Nchi na kupanua wigo wa biashara ndani na nje ya Nchi.
Mhe. Kindamba amesema hayo Agosti 8, 2023 wakati wa kilele cha maadhimisho ya Nanenane Kanda ya Mashariki 2023 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo Manispaa ya Morogoro Mkoani humo.
“Maonesho ya shughuli za kilimo, Mifugo na Uvuvi yaani Nanenae kwa mwaka huu ni muhimu sana katika kuinua sekta hizi; kwani yanawezesha wakulima na Wafugaji kupata elimu kuhusu kilimo bora, kuongeza uzalishaji wenye tija, kupanua wigo wa masoko pamoja na kuongeza mtandao wa mahusiano baina ya Wakulima na Wadau wengine zikiwepo taasisi za Kifedha ambazo zinatoa fursa za mikopo kwa wakulima na Wafugaji”. Alisema Mhe. Kindamba.
Mhe. Kindamba alisema kupitia maonesho hayo shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi zitaleta tija kwa kujifunza teknolojia na mbinu za kisasa zinazoendana na mabadiliko ya tabia nchi kwani kwa kuongeza uzalishaji kupitia teknolojia mpya iliyotolewa Katika maadhimisho hayo itakuwa rahisi kupata masoko ya mazao hayo.
"Tutaweza kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji kwa ajili ya mahitajiya nchi yetu na ziada kwa ajili ya kuuza nje ya nchi Sina shaka na wakulima, wafugaji na wavuvi na wadau wote ambao tumepata fursa ya kutembelea Maonesho haya tumejifunza teknolojia na mbinu mpya ambazo tukizitumia vizuri zitasaidia kuongeza uzalishaji". Alibainsha.
Amesisitiza kuwa teknolojia hizo za kilimo, ufugaji na uvuvi ziweze kuwafikia wakulima katika maeneo yao ili kuongeza ufanisi katika kazi na kutoa wito kwa sekta za umma na binafsi kushirikiana vyema na wakulima ili maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki kuendelea kuboreshwa kwa kuhimiza wadau kuleta teknolojia zitakazowapa elimu wakulima wa Kanda hiyo.
Aidha Mhe. Kindamba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kwa kuongeza bajeti ya kilimo na kutoa ruzuku pamoja na kupunguza bei za viwatilifu na mbolea;na kwamba Mhe Rais amefikia uamuzi huo kwa kutambua wa wakulima wenye hali ya chini ili kupata pembejeo hitajika hivyo kupata mazao ya kutosha.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima Kwa niaba ya wanakamati wa Maonesho hayo Kanda ya Mashariki amewashukuru wadau mbalimbali wakiwemo Bodi ya sukari Kwa kujitoa kufanikisha Maonesho hayo.
Mhe. Malima ameongeza kuwa wadau mbalimbali ambao walitakiwa kuongeza nguvu wajipange ili Maonesho yajayo yawe Bora zaidi na kutaka kuwa na vipando vya kudumu vya Maonesho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa