Wazee Wilayani Gairo wamekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya Mhe. Jabir Omary Makame ambapo walielezea kero mbalimbali zinazo wakabili.
Juni 23 2021 walikutana kwa pamoja na Mhe. JOM katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ambapo mbali na maswala mengine kilio chao kikubwa kilikuwa ni ukosefu wa Dawa kwa Wazee katika kituo cha Afya Gairo.
Wazee hao walimwambia Mkuu wa Wilaya kuwa wanapofika kituoni hapo kwa ajili ya kupata huduma za afya wamekuwa wakielekezwa na madaktari kuwa hakuna dawa na kuwataka wakanunu kwenye maduka yaliyopo nje hali ambayo walisema hawana uwezo wa kugharamia matibabu na ununuzi wa dawa.
Akijibu hoja zao Mhe. JOM alimtaka Mganga Mkuu wa Wilaya Dakta Danstan Mshana kutoa maelezo kuhusu malalamiko hayo ambapo Dakta Mshana aliskiri kuwepo na changamoto ya upungufu wa dawa kwa kipindi cha nyuma na kwamba changamoto hiyo ilishapata ufumbuzi wake.
Dakta Mshana alibainisha kuwa changamoto ya upungufu wa dawa kituoni hapo inasababishwa na Mzabuni ambaye ni Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD) mwenye jukumu la kusambaza dawa Nchini analeta dawa pungufu tofauti na mahitaji yaliyoombwa hivyo kusababisha kuwepo na upungufu huo.
“Mhe. Mkuu wa Wilaya ni kweli kabisa malalmiko ya Wazee wetu kuhusu upungu wa dawa pale kituoni, kiasi cha dawa tunazo agiza MSD na kiasi kinacho letwa ni tofauti kabisa kunakuwa na upungufu mkubwa, lakini pia Kituo cha Afya Gairo kinatoa huduma kama Hospitali ya Wilaya hivyo inapokea wagonjwa wengi kuliko uwezo wake”. Alibainisha Dakta Mshana.
Kwa upande wake Mhe. JOM aliwambia Wazee hao kuwa amesikia na kupokea changamoto zao na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na Wataalam wa Halmashauri ili kuhakikisha changamoto zao zinapata utatuzi kwa haraka.
“Kwanza ninawashukuru sana Wazee wangu kwa kukubali kuja kunisikiliza na kunipokea, nina ahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha lakini pia nitahakikisha changamoto zenu zote zilizo ndani ya uwezo wangu zinapata ufumbuzi, zingine ni za kisera zaidi nazo tutazifikisha mahali panapo husika”. Mhe. JOM aliwambia.
Mhe. JOM amekutana na Wazee hao ikiwa ni siku ya tatu tangu kuwasili Wilayani Gairo ambapo kwa mara ya kwanza aliwasili Gairo Juni 22,2021 ambapo alikutana na kufanya kikao na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kisha kushiri kikao cha kamati ya Sherehe Wilaya kujadili maandalizi ya mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021.
WAZEE WILAYANI GAIRO WAELEZA KERO ZAO DC MPYA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa