• Mawasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
GAIRO DISTRICT COUNCIL
GAIRO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Authorities Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira
    • Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni za Halmashauri
      • Seksheni ya Rasilimali Watu
      • Seksheni ya Utawala
    • Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Baraza la Madiwani
  • Miradi
    • Miradi ya Maendeleo
      • Sekta ya Elimu Msingi
        • Miradi Mipya
        • Miradi iliyokamilika
      • Sekta ya Elimu Sekondari
      • Sekta ya Afya
      • Sekta ya Barabara/Miundombinu
      • Sekta ya Maji
  • Machapisho
    • Katiba ya JMT
    • Sheria ndogo ndogo za Halmashauri
    • Hotuba Mbalimbali
    • Sera ya Elimu
    • Taarifa za Hesabu za Mwisho
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

WIZARA YA KILIMO ZANZIBAR KUIMARISHA USHIRIKIANO NA MKOA WA MOROGORO

Posted on: August 5th, 2023

Na. Cosmas Mathias Njingo. MOROGORO

Agosti 5.2023

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis, amesema Wizara yake ipo tayari kushirikana na wataalam, wakulima na viongozi wa Mkoa wa Morogoro katika kuongeza uzalishaji wenye tija wa mazao ya kimkakati hususan zao la karafuu kwa lengo la kuinua uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla.

Mhe. Shamata ameyasema hayo Agosti 3, 2023 alipotembelea banda la Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ambayo inalima zao karafuu wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Nanenane yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mjini Morogoro.

Aidha, Mhe. Shamata Khamis amesema kutokana na umuhimu wa zao hilo katika kukuza kipato cha wakulima na taifa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya kilimo itashirikiana na Mkoa wa Morogoro kwa karibu zaidi na kuhakikisha mazao hayo yanakuwa na tija. Kwa msingi huo, Wizara hiyo inatoa nafasi kwa wataalam na wakulima kutoka Mkoani Morogoro kwenda Zanzibar kupata elimu na ujuzi wa uzalishaji wa mazao hayo.


“Nitoe wito tuendelee kuungana, kushirikiana kubadilishana wataalam, kufanya vikao vya pamoja ili kuhakikisha mazao haya yanakuwa na tija ya uzalishaji” amesema Mhe. Shamata Shaame Khamis.

Sambamba na hilo, Mhe. Shamata wakati akiwa kwenye banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) amesisitiza watendaji wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa weledi na kwa ushirikiano ili kutimiza lengo la serikali katika ukusanyaji wa mapato.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amemshukuru Waziri huyo kwa kutembelea maonesho hayo Kanda ya Mashariki na kukubali kupokea wataalam ambao watapata uzoefu juu ya uzalishaji wa mazao ya kimkakati hususan zao la karafuu.

Mhe. Malima ameongeza kuwa itaundwa timu ya wataalam 30 wakiwemo wakulima 20, maafisa kilimo 5, waandishi wa habari 5 ambao wataenda kujifunza namna bora ya uzalishaji wa karafuu, aidha, amesema ziara ya Waziri huyo itafungua fursa za kilimo kwa wakulima wa Kanda ya Mashariki.

Kwa niaba ya waoneshaji, Bw. Abdalah Mkazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ambaye ana ulemavu wa macho amesema maonesho ya Nanenane 2023 hayajawaacha nyuma watu wenye ulemavu ambapo imetoa fursa kwao kuonesha ujuzi walionao, hivyo ameishukuru Serikali ya Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia nafasi hiyo. Ameongeza kuwa amebuni kifaa cha kuingiza uzi kwenye sindano kitakacho wasaidia

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUITWA KWEYE USAILI WAOMBAJI NAFASI ZA AJIRA MTENDAJI WA KIJIJI III NA DEREVA II September 21, 2024
  • TANGAZO LA HALMASHAURI KUKUSANYA USHURU WA USAFI May 07, 2024
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA PROGRAM YA BBT May 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA DEREVA July 12, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAJALIWA AFUNGUA TAWI LA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR MKOA WA MOROGORO

    July 17, 2024
  • GAIRO SEKONDARI YATEKELEZA AGIZO LA KULIMA BUSTANI ZA MBOGAMBOGA, MATUNDA

    July 15, 2024
  • MARUFUKU KUUZA, KUNUNUA MAZAO KWA KUPIMA KWENYE NDOO, MADEBE

    July 12, 2024
  • KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI

    July 11, 2024
  • Tazama zote

Video

WANAFUNZI DARASA LA SABA WAASWA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni za Manunuzi
  • Zabuni za Ujenzi
  • Huduma

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Tanzania
  • GAIRO ONLINE TV
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Mawasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.

    Sanduku la Posta: 40, GAIRO

    Simu ya Mezani: +255 787730665

    Simu ya Kiganjani: +255 717222572

    Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa