Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhe. Rachel Nyangasi amewataka waheshimiwa Madiwani wote kutoa ushirikiano kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu Asajile Lucas Mwambambale pamoja na wakuu wa idara na vitengo kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo la kukusanya shilingi bilioni 1.084 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Ametoa kauli hiyo wakati akitoa salamu kwa wajumbe wa Kamati ya Huduma za jamii wakati wa kikao cha Kamati hiyo kinacho jumuisha baadhi ya Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wataalamu kutoka Idara na Vitengo vya Halmashauri kilichofanyika Agasti 19.2021 katika ukumbi wa Halmashauri.
Mhe. Nyangasi alisema kukusanya mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kutoka kwenye milioni 730,000,000 zilizokisiwa katika mpango wa bajeti unaotekelezwa hivi sasa wa mwaka wa fedha 2021/2022, inawezekana kwa kuweka nia ya dhati na kujituma kutekeleza mkakati huo wa kukusanya mapato kupitia vyanzo vya mapato yasiyolindwa.
“Waheshimiwa Madiwani, kwa hili tunahitaji kuwa kitu kimoja tushirikiane na Mkurugenzi wetu pamoja na wataalam wake ili tuongeze nguvu ya pamoja katika kuinua Halmashauri yetu kwenye mapato, nina uhakika nguvu ya pamoja itatuwezesha kufikia lengo la kukusanya Shilingi bilioni moja na zaidi, haya yote yatawezekana tukiwa na nguvu moja, kauli moja, luga moja pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana”, alisisitiza Mhe. Nyangasi.
Aliwataka Waheshimiwa Madiwnai hao kuwa mfano wa kuigwa na Wananchi wanao waongoza kwa kulipa ushuru kupitia bishara wanazofanya ili kuiongezea Halmshauri kipato badala ya kutumia vibaya nyadhifa zao kukwepa kulipa kodi za Serikali.
“Nawaomba sana Waheshimiwa na sisi tujifunze kulipa kodi za Serikali kwa hiari yetu bila kusubiri kushurutishwa au kupigwa faini kwa kushindwa kuetekeleza wajibu wetu, si jambo jema wala haipendezi kuona Mheshimiwa Diwani anatozwa faini kwa kosa la kusafirisha bidhaa za mazao ya kilimo bila kulipia ushuru, kwanza ni aibu pili haileti picha nzuri kwa tunao waongoza”. Mhe. Mwneyekiti wa Halmashauri aliwasihi Madiwani hao.
Mweyekiti huyo wa Halmashauri akatumia nafasi hiyo kumwagiza Mgaga Mkuuwa wa Wilaya Dakta Dastan Mshana kusimamia makusanyo ya mapato yatokanayo na huduma za afya kwenye kituo cha afya na zahanati zote kupitia mfumo wa taarifa za afya
GoT-HOMIS ambao unatumika kwenye vituo vya kutolea huduma nchi nzima.
“Kuna mapato yanavuja kwenye kituo chetu cha afya na zahanati. Naagiza Mganga Mkuu kuhakikisha unasimamia mapato na kudhibiti matumizi hewa, hii iende sambamba na matumizi sahihi ya mfumo wa Got-HOMIS kwenye zahanati zote na kituo cha Afya Gairo.
Awali akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kutoa nasaha zake na kusalimia wajumbe wa kamati hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ndugu Asajile Lucas Mwambambale aliwambia Waheshimiwa Madiwani kuwa msingi wa kuanzishwa kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni kushusha huduma karibu kwa Wananchi walipo na kurahisisha utatuzi wa kero zao”
“Msingi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ni moja tu, kuwahudumia Wananchi wake kwa urahisi na kutatua kero zao kwa haraka zaidi. Na matarajio ya Kiongozi wetu Mkuu wa Nchi Mhe. Mama Samia Suluhu Hassani, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuona watendaji alowateua wanamsaidia kutekeleza majukumu ya kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kuwahudumia Wananchi wake”, alieleza Mwambambale.
Mkurugezi Mwambamali alisema swala la kutekeleza ilani ya Chama Tawala siyo jambo la mtu mmoja bali linahitaji ushirikiano kutoka kwa viongozi wa ngazi zote ikiwepo Waheshimiwa madiwani, wakuu wa idara, na kwamba aliwaomba Waheshimiwa Madiwani, watumishi na jamii nzima kumpa ushirikiano wa kila namna ili kumuwezesha kufikia lengo lake la kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo vilivyopo nje ya mpango wa bajeti ya mwaka 2021/2022.
Akasema, “Ninawaomba sana mnipe ushirikiano wenu wa kutosha ili utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi uwe rahisi kwetu sote kwa kukidhi matarajio ya Kiongozi wetu na matarajio ya Wananchi ambao wamewapa dhamana kubwa na imani waliyonayo kwenu Waheshimiwa Madiwani”.
Akasisitiza kuwa si jambo jema Waheshimiwa Madiwni na watendaji wa Halmashauri kuendelea kukiri udhaifu wa ufinyu wamakusanyo ya mapato na badala yake kufikiria mbali zaidi katika kuibua vyanzo vipya nje ya mpango wa bajeti unaotekelezwa wa 2021202 ili kuiwezesha Halmashauri kukusanya zaidi ya makadirio ya sasa ya shilingi milioni 730,000,000,000.
“Waheshimiwa Madiwani, kuendela kuzungumza kuwa sisi ni wadogo ni sawa na kukiridhi udhaifu kuwa uwezo wetu wa makusanyo umeishia hapo hakuna namna nyingine ya kukua, hili siyo sawa ni wakati wa kubadilika na kuzungumza kuwa Gairo ni kubwa kwani nimedhamiria kuona tunatoka hapa tulipo na kufikia kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa mwaka huu wa fedha wa 2021/2022”. Alitanabahisha Mkurugenzi Mwambambale.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa