Msisitizo umekuwa ukitolewa kwa Watendaji wa Kata, Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi kuhakikisha Shule zote zinatoa chakula cha mchana sambamba na kulima bustani za Mbogamboga na Matunda ili kuwezesha Wanafunzi kupata mlo kamili na Lishe Bora kwa lengo la kujenga afya zao
Shule ya Sekondari Gairo imetekeleza Agizo hilo kwa vitendo kwa kuanzisha bustani ya matunda na mbogamboga
Uongozi wa Shule yà Sekondari Gairo umedhamiria kuhakikisha Wanafunzi wake wanapata Lishe Bora kwa kuwekeza kwenye Kilimo Cha bustani ya Mbogamboga namatunda pamoja na kuwafundisha Wanafunzi wao somo la maarifa ili kuwajengea uwezo wa kuwa na utamaduni wa kutumia vyakula vyenye Lishe itokanayo na makundi 5 ya vyakula..
Pichani aadhi ya Wanafunzi na Mwalimu wao wakiendelea na zoezi la utunzaji wa bustani yao ya Mbogamboga na Matunda kwa kurudishia mbegu katikasehemu ambazo hazikuota, lengo ni kuhakikisha Kilimo hicho kinaleta tija kwa Wanafunzi hao na Walimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa