MOROGORO
Julai 9.2024
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) ameutaka uongozi wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) kutoa Elimu kwa umma kuhusu uwekajiakiba na mikopo yenye masharti nafuu, sambamba na kuelezea utendaji kazi wake ili kuhamasisha Wananchi kutumia huduma za Benki hiyo katika kukuza Uchumi wao.
Mhe. Majaliwa ametoa agizo katika hafla ya ufunguzi wa Tawi la Benki ya PBZ iliyofanyika Mtaa wa Nunge Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mkoani humo Julai 9, 2024, ambapo ameusisitiza Uongozi wa Tawi la Benki hiyo kuelezea kwa kina kuhusu huduma za kifedha zinatakzo tolewa na Benki ya PBZ.
“Mnawajibu mkubwa wa kuhakikisha mnatoa Elimu kwa wadau kuhusu huduma zenu za kifedha, masharti ya mikopo, upatikanaji wake, riba, urejeshaji na usimamizi wa mikopo hiyo. Hii ni muhimu sana kwa Wananchi na Wadau wengine, kwani wakishajua huduma zinazotolewa na PBZ itawawezesha kufanya maamuzi na uchaguzi sahihi wa kutumia huduma zenu.” Alsisitiza Mhe. Waziri Mkuu.
Kwa upande mwignine Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa amewahimiza Wananchi kutumia fursa ya uwepo wa Tawi la PBZ kujikwamua kiuchumi kupitia huduma za kifedha za Benki hiyo, ikiwepo kukuza kitaji kwa kupata mikopo nafuu ya kuanziasha au kuendeleza Biashara zao na kuwsisitiza wajasiliamali Wadogo kufungua akaunti na kuweka akiba katika Benki hiyo ili wapate kunufaika na huduma za mikopo.
“Kufunguliwa kwa Tawi la benki hiyo Mkoani Morogoro inasogeza fursa kwa Wananchi kuingia kwenye ujasiliamali kwa kukopa na kufanya shughuli za uzalishaji, ni wakati muafaka kwa Wajasiliamali kufungua akaunti kwenye tawi la PBZ, kuweka akiba mara kwa mara na kuzingatia masharti ya mikopo mtakayokopa ikiwemo sharti kurejesha kwa wakati wa mikopo hiyo”. Alissema.
Aidha Waziri Mkuu amempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake mahiri wa kufungua fursa za uwekezaji hususani Sekta Binafsi kusogeza huduma za kifedha kwa Wananchi kupitia na kwamba Taasisi hizo za kifedha hususani Mabenki, ikiwepo PBZ zinazochagiza kukua kwa Uchumi wa Nnchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa