Na, Cosmas Mathias Njingo
GAIRO, Morogoro
Sepetemba 25.2022
Wananchi wanakabiliwa na vikwazo mbalimbali katika kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za uchumi, ikiwepo Upatikanaji wa mitaji, Ukosefu wa ujuzi na uzoefu; vikichochewa na upungufu katika elimu, mafunzo, mila na desturi potofu na mtazamo wa kimaendeleo.
Diwani wa Kata ya Gairo Mhe. Danistan Mwegoha (mwenye shati jeusi) akikabidhi kadi ya pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja wa Walemavu Gairo Bw. Dikson Msagala (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Kwa kutambua hilo, mnamo mwaka 2004 Serikali ikatoa mwongozo kupitia Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, kwa kukakikisha inaweka mazingira rafiki kwa Wananchi wake, kupata mitaji kupitia mikopo yenye mashariti nafuu ili waweze kubuni na kuanzisha shughuli za uzalishaji mali zitakazo wasaidia kujikwamua kiuchumi na kupata kipato cha kuendesha maisha yao.
Uwezeshaji huo pia ililenga kutatua changamoto za Ukosefu wa masoko ya uhakika au uwezo wa kuingia katika masoko yenye ushindani, Ukosefu wa ushirikiano, ushirika hafifu na ukosefu wa sauti ya pamoja ya makundi mbalimbali ya wananchi katika kusimamia maslahi yao, na kukabilina matatizo yanayowakwaza wasishiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi katika sekta mbalimbali.
Baadhi ya Viongozi na Wajumbe wa Kikundi cha Umoja wa Walemavu Gairo katika picha ya pamoja baada yakukabidhiwa kadi pikipiki ya miguu mitatu ya kubeba mizigo (bajaji) baada ya kukamilisha kulipa deni la mkopo wa sh.8,500,000.(Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Katika mwaka wa Fedha 2020/2021 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, dawati la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi ilitoa Mkopo wa 10% unaotokana na mapato yake ya ndani, kwa Vikundi tisa (09) vya Wanawake, viwili (02) Vijana, na Vitatu (03) Watu Wenye Ulemavu, jumla ya Shilingi 104,771,000.
Moja ya vikundi vilivyonufaika na sehemu ya Mkopo huo wa 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri, ni kikundi cha Umoja wa Walemavu Gairo, ambacho awali kilipata Mkopo wa shilingi laki nane (800,000), baada ya kurejesha kiasi hicho cha fedha, kikaomba tena mkopo mwingine ili kuendeleza harakati za kujikwamu kiuchumi kupitia shughuli za uzalishaji mali.
Kikundi cha Umoja wa Walemavu Gairo kilikopeshwa Jumla ya Shilingi milioni nane na laki tano (8,500,000), ikiwa ni sehemu ya mkopo wa 10% wa kuwezesha makundi ya Wanawake (4%), Vijana (4%) na Watu wenye Ulemavu (2%). Ambapo mkopo huo wa mashariti nafuu hurejeshwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa kutegemeana na thamani yake na masharti ya mkopo husika.
Kiti ya fedha hizo kiasi cha Shilingi milioni sita na laki tani (6,500,000) zilitumika kununulia Pikipiki ya Kukeka mizigo ya miguu mitatu maarufu Guta, na kiasi kilichosalia cha Shilingi milioni mbili (2,000,000) kilitumisha kukamilisha taratibu mbalimbali ikiwepo usajili wa Guta hilo.
Kikundi cha Umoja wa Walemavu Gairo kimekabidhiwa rasmi Kadi ya Pikipiki ya Miguu mitatu ya kubeba mizigo maarufu Guta, baada ya kukamilisha marejesho na kutimiza masharti ya mkopo wa 2% kwa watu wenye Ulemavu unaotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akizungumza wakati wa mabidhiano ya Kadi ya Guta hilo mbele ya baadhi wa wajumbe wa Umoja wa Walemavu Gairo, Diwani wa kata ya Gairo na Mjumbe wa Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango Halmashauri, Mhe. Dinistan Mwegoga alisema utaratibu wa kurejesha 10% ya mapato ya ndani kwa Wananchi ni mkombozi katika kutatua changamoto za kiuchumi zinazowakabili Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.
“Naipongeza sana Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza utaratibu huu wa kuwezesha kiuchumi makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo 10% hutengwa na kurudishwa kwa wananchi kupitia mwenye makundi ya uzalishaji mali”. Alisema Mhe Diwani Mwegoha.
Naye Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendelo ya Jamii Bw. George Katoto alikipongeza kikundi hicho kwa kurejesha mkopo huo ndani ya wakati na kuvitaka vikundi vingine kuwa waaminifu kwa kuhakikisha mikopo yao inarejeshwa ili kusaidia vikundi vingine kukopa.
“Nawapongeza sana kikundi cha Umoja wa Walemavu kwa kukamilisha kulipa mkopo wao ndani ya Wakati, wito wangu kwa vikundi vingine ambavyo bado havijakamilisha marejesho kuiga mfano huu ili vikundi vingine navyo viweze kunufaika na fursa hii ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi”. Alisistiza Bwn. Katoto.
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Msifwake Haule alisema kazi kubwa ya Divisheni yake ni kuweka maoteo ya ukusanyaji wa vyanzo vya ndani vya mapato ya Halmashauri, kupanga na kusimamia utekeleza bajeti, pamoja na kuhakikisha 10% ya sehamu ya mapato ya ndani inarudi kwa kwa Wananchi.
“Wajibu wetu mkubwa ni kuhakikisha tunasimamia mapato yetu ya ndani, na asilimia 10 yake inarudi kwa Wananchi ili kuwezesha makundi ya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu. Na hapa mbele yetu ni Wanakikundi wa Umoja wa Walemavu ambao wamenufaika na sehemu ya asilimia 10% kwa kupata asilimi mbili kwa ajili ya kuwezesha walemavu”. Alimema.
Bi. Stella Simon Ngomano ni Afisa Maendeleo ya Jamii kitengo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, anaeleza kuwa Kikundi cha Umoja wa Walemavu Gairo kimeonyesha uaminifu mkubwa katika kurejesha mkopo huo na kwamba Halmashauri inakabidhi rasmi Kadi ya Guta hilo ili kuwapa umiliki halali wanaumoja wa kikundi hicho.
"Tunawapongeza Wanaumoja Huu wa Kikundi wa Walemavu Gairo, kwa uaminifu wao mkubwa katika kufanya marejesho ya mkopo wa Shilingi milioni nane, wamerejesha kwa wakati hivyo nasi kama tunawakabidhi rasmi Kadi ya umiliki halali wa Guta lao". Alisema Bi. Ngomano.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho Bw. Dikson Msagala akaishukuru Serikali kwa sera zake madhubuti za kuwezesha Wananchi wake Kiuchumi na kupongeza Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kwa kutoa Mkopo huo ambao alisema kuwa umewasaidia kupata kipato na kujikwamuwa kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa