Mratibu wa zao la tumbaku wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Ndugu.Shigela Shinyanga ametaja kuwepo kwa mkakati wa kuzalisha zaidi ya tani 600 kwa zao la tumbaku katika msimu wa kilimo ujao kwa mwaka 2025/2026 wilaya ya Gairo.
Ameyasema hayo katika kikao cha wadau wa zao hilo cha kujadili kilimo cha tumbaku kwa Msimu wa mwaka 2025/2026 kilichofanyika septemba 12.2025 kwenye ukumbi wa mikutani wa ofisi ya mkuu wa Wilaya.
Shinyanga ambaye pia ni Afisa Kiimo makao makuu ya Halmashauri, amesema kuwa matarajio ya uzalishaji ni makubwa kutokana na kile kilichopatikana katika majaribio kuleta matokeo chanya , ambapo hadi saaa zaidi ya wakulima 300 wamepatiwa Elimu ya zao la tumbaku huku pembejeo za awali kwa msimu ujao wa kilimo zimetolewa sambamba na kalenda itakayowaongoza wakulima na maafisaugani ngazi za kata kutekeleza shughuli za uzalishaji bila kuwa na kikwazo cha ucheleweshaji kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande mwingine, Afisa Kilimo huyo, ametaja kuwepo kwa ushirikiano mkubwa kutoka wa taasisi za fedha ikiwepo Benki kwa utoaji wa mikopo ya kuwawezesha wakulima wa zao la tumbaku kupata pesa za kuendesha kilimo, uzalishaji na kuongeza kuwataasisi hizo za fedha zinaenddela kutoa elimu kwa wakulima kuhusu upatikanaji wa mkopo kupitia Amcos zao.
Kwa mujibu wa Mratibu huyo, Halmashauri ya Wilaya ya Gairo inatarajia kufikia wa kulima zaidi ya 500 kutoka kata 14 zinazotarajiwa kulima zao la tumbaku ambapo kila kata itasajili wakulima zaidi ya 40 wa zao hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa