Mshauri wa uzalishaji wa zao la Tumbaku kutoka Shirika la mkwawa leaf tobacco ndugu .Louis Roussos ametaja kuwapatia wakulima wa zao la tumbaku pakti mbili za mbegu kwa kila hekta moja bila gharama yeyote ili kuchagiza uzalishaji wa zao hilo Wilaya ya Gairo.
Amesema hayo Septemba 12.2025 katika kikao cha Wadau wa zao la tumbaku cha kujadili kilimo cha tumbaku kwa mwaka 2025/2026 Kilichofanyika katika Ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Ndugu Louis amesema kuwa Mkwawa leaf kwa kushirikiana na Uongozi na wataalam wilaya ya Gairo wamedhamilia kuongeza na kuitambulisha Gairo kupitia uzalishaji wa zao la tumbaku.
Akitoa elimu fupi namna bora ya kuchoma tumbaku hiyo kwa kutumia mvuke wa jua ndugu louis amesema njia hii ya nishati safi ya kukaushia tumbaku ni rafiki kwani Ina punguza gharama kubwa ukilinganisha na ile ya kukausha na moto sambamba na utunzaji wa mazingira.
Wilaya ya Gairo inatarajia kuzalisha tani 672 kwa hekta 560 kwa mwaka 2025/2026 na hivyo kuongeza mapato ya Halmashauri na kuimarisha uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja kupitia Sekta ya kilimo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa