Kikao cha menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kujadili na kupitia taarifa Za Agost.2025 kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri leo Sept.12.2025.
Katika kikao hicho menejimenti imepitia na kujadili kuhusu mapato na Matumizi ya Halmashauri kwa mwezi agost.2025 mwenendo wa sekta ya biashara kwa mwezi agost na taarifa ya kupokea maombi ya Wadau wa uwekezaji katika wilaya ya Gairo sambamba na jitihada na mikakati mbali mbali ya kuongeza hali ya ukusanyaji wa mapato hasa katika kipindi cha Msimu wa uuzaji wa mazao ya kilimo ambapo Wilaya ya Gairo inategemea mapato makubwa kutoka katika sekta ya kilimo.
Aidha menejiment imepitia na kujadili Mpango mkakati wa kukuza Sekta ya utalii ambapo uhamasishaji kuhusu ziara ya kutembelea hifadhi ya ukaguru kuendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na matangazo katika vyombo vya habari ili kuwawezesha wananchi kujua vivutio vinavyopatikana katika wilaya ya Gairo ili kuendelea kuvutia wataliii kutoka nje na ndani ya Nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa