Na Cosmas Njingo, GAIRO DC
Rai imetolewa kwa Waheshimiwa Madiwani wa Halmashaui ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na mshikamano wa karibu kati yao na Watendaji wa kata na vijiji katika kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwepo miradi ya kimkakati pamoja na kushiriki kikamilifu kwenye kukusanya na kusimamia mapato kwenye maeneo yao ili kuziba mianya inayosababisha kupotea kwa makusanyo ya Serikali.
Rai hiyo imetolewa na Mheshimiwa Rahel Nyangasi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, wakati akifungua Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani kujadili taarifa za Utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2021/2022. Mkutano uliofanyika Mei 20.2022 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
“Waheshimiwa Madiwani ninawaomba tuache kuibua migogoro na marumbano kati yetu na Watendaji wa kata, tujenge mahusiano bora na tukafanye kazi kwa ushirikiano mkubwa na Watendaji wetu hasa katika kusimamia shugulizi za ukusanyaji mapato pamoja na kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,hii itasaidia kuongeza kasi katika uwajibikaji na kuimarisha mahusiano kati yetu na watendaji wa Serikali”, afafanua Mwenyekiti huyo.
Mheshimiwa Nyangasi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Chigela aliwambia Waheshimiwa Madiwani hao kwamba kujenga mahusinao bora na kuimarisha ushirikiano baina yao na Watendaji wa Kata na Vijiji ni swala muhimu katika kuboresha ustawi wa afya ya kuwaletea maendeleo Wananchi kwani mahusiano na mashirikiano hayo yanasaidia kutekeleza majukumu yao kwa kizingatia sera, sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za Serikali za Mitaa.
‘Moja ya vitu muhimu vinavyo imarisha afya ya maendeleo katika kata zetu ni kuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya Mheshimiwa Diwani na Watendaji wa Serikali kwenye kata husika, kwa pamoja ni vyema tuhakikishe mahusiano yetu na Watendaji yanaimarika ili tuweze kushirikiana kusimamia kutekeleza wa shuguli za mandeleo ikiwepo ukusanyaji wa mapato”. alisisitiza Mhe. Nyangasi.
Akitoa salam za Chama, Menyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Ndugu Shabani Sajio alionya tabia ya baadhi ya Waheshimiwa Madiwani hao kujiingiza katika migogoro na watumishi ikiwepo Watendaji wa kata huku baadhi yao wakifikia hatua ya kuwakataa na kudai kwa Mkurugenzi kuwahamisha Watendaji hao.
“Nimesikia kuna baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wamejiingiza kwenye migogoro na watendaji wao wa kata, na kibaya zaidi wamefikia hatua ya kumlazimisha Mkurugenzi wa Halmashauri kuwahamisha vituo vya kazi Watendaji, hii ni sawa haiubaliki. Achene tabia ya kujiingiza kwenye migogoro isiyo na tija kwa wananchi kwani mnachelewesha maendeleo”. Ndugu Sajilo alikemea.
Alisema kuhamisha watendaji kutoka kata moja kwenda nyingine kwa sababu ya migogoro baina yao na Waheshimiwa Madiwani siyo njia bora ya kutatua tatizo badala yake akashauri kutoa taarifa kwa mamlaka zao za kinidhamu ikiwepo Kamati ya Siasa ya Chama Cha mapinduzi Wilaya ili iwashugulikie kwa mujibu wa sheria na taratibu.
“Kama kuna watendaji siyo waadiifu, wasiotimiza majukumucyao kikamilifu na kwa weledi, wengine hawapendi kukaa kwenye vituoa vyao vya vya kazi, hawa Mamlaka yao ya nidhamu ni Mkurugnzi, akishindwa yeye tuleteeni sisi majina yao kwenye Kamati ya Siasa ya Chama tutajua njia sahihi za kuwashughuikia endapo Mkurugnzi wa Hamashauri atashinda kufanya kazi yake ya kuachukulia hatua za kinidhamu’. Alisisitiza Mwenyekiti Sajilo.
Wajumbe wa Mkutano huo wa Baraza la Kawaida la Waheshimiwa Madiwani, mbali na kujadili utekelezaji wa taarifa za robo ya tatu kwa kipindi cha Januari Machi 2021/2022, walikubaliana kwa kauli moja na kuweka azimio la kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi yake ya kuboresha maslahi kwa watumishi wa Umma aliyoitoa Mei Mosi 2021 katika Sherehe za maadhimisho ya Wafanyakazi Dunia, kwenye Viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza, ambapo katika maadhimisho ya sherehe hizo mwaka Huu Rais Samia alitangaza kutimiza ahadi yake na baadae mapema hivi karibuni Serikali ikatangaza nyongeza ya 23.3 ya kima cha chini cha mshahara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa