(Christopher Walles Mussa, Afisa Kilimo na Mratibu wa Mpango wa kudhibiti Sumukuvu Wilaya ya Gairo kupita Mradi wa TANIPAC akielezea madhara ya sumukuvu kwa Binadamu na Mifugo, kwenye kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo kupitia Rasimu ya Shelia Ndigo za Halmashauri za kudhibiti sumukuvu)
Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Christopher Walles Mussa, Afisa Kilimo na Mratibu wa Mpango wa kudhibiti Sumukuvu Wilaya ya Gairo kupita Mradi wa TANIPAC ameeleza hayo wakati wa kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo kupitia rasimu ya Sheria ndogo za kudhibiti sumukuvu kilichofanyika Julai 6 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
(Christopher Walles Mussa, Afisa Kilimo na Mratibu wa Mpango wa kudhibiti Sumukuvu Wilaya ya Gairo kupita Mradi wa TANIPAC akielezea madhara ya sumukuvu kwa Binadamu na Mifugo, kwenye kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo kupitia Rasimu ya Sheria Ndigo za Halmashauri za kudhibiti sumukuvu)
"Sumukuvu ina madhara makubwa sana kwa binadamu na mifugo endapo watatumia vyakula vilivyo athiriwa na sumukuvu', Alisema Bwana Walles
Akitaja madhara hayo Mratibu huyo wa kudhibiti sumukuvu alisema ni pamoja na Kansa, kudumaa kiakili na kimwili kwa watoto wadogo na kusababisha vifo.
(Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakijadili Mswaada wa Sheria Ndogo ya Halmashaurii ya Kudhibiti Sumukuvu Wilayani Gairi)
"Vifo ni mojawapo ya madhara yatokanayo na sumukuvu ikiliwa kwa kiwango kingi, lakini ikiliwa kwa kiwango kidogo kidogo, mlaji anawenza kupata Kansa, na watoto wadogo kudumaa kimwili na kiakili". Alifafanua Bwana Walles.
Alibainisha kuwa binadamu anaweza kupata athari kutokana na kunywa maziwa, kula Maini na figo au vyakula vya nafaka aina ya mahindi na karanga.
Alisema maziwa, maini na figo huathiriwa na sumukuvu endapo mifugo itakula mazao yaliyo athiriwa na sumu inayotokana na kuvu.
(Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakijadili Mswaada wa Sheria Ndogo ya Halmashaurii ya Kudhibiti Sumukuvu Wilayani Gairi)
Aidha alieleza kuwa sumukuvu ni aina sumu inayotokana na ukungu (fangasi) wa mimea na mazao inapatikana kutokana na mfumo mbovu wa ukaushaji, uhifadhi na usafirishaji wa mazao.
Hata hivyo ameitaka jamii ya wafugaji na wakulima kuepuka kulisha mifugo yao mazao yenye viashiria vya kuvu ili kuzuia madhara ya sumukuvu kwa binadamu na mifugo pamoja na kuto safirisha, kausha au kuanika mazao kwa njia zisizo kubalika
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa