• Mawasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
GAIRO DISTRICT COUNCIL
GAIRO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Authorities Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira
    • Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni za Halmashauri
      • Seksheni ya Rasilimali Watu
      • Seksheni ya Utawala
    • Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Baraza la Madiwani
  • Miradi
    • Miradi ya Maendeleo
      • Sekta ya Elimu Msingi
        • Miradi Mipya
        • Miradi iliyokamilika
      • Sekta ya Elimu Sekondari
      • Sekta ya Afya
      • Sekta ya Barabara/Miundombinu
      • Sekta ya Maji
  • Machapisho
    • Katiba ya JMT
    • Sheria ndogo ndogo za Halmashauri
    • Hotuba Mbalimbali
    • Sera ya Elimu
    • Taarifa za Hesabu za Mwisho
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

BILIONI 8 KUIMARISHA MPANGO WA MAFUNZO WA MADAKTARI BINGWA NA BOBEZI NCHINI. Na. Cosmas Mathias Njingo CHANZO; https://www.moh.go.tz/news Oktoba 28.2022 Serikali kupitia Wizara ya Afya imeongeza fedha za kusomesha Wataalamu bingwa na bobezi hadi kufikia

Posted on: October 31st, 2022

Na. Cosmas Mathias Njingo

CHANZO; https://www.moh.go.tz/news

Oktoba 28.2022

Serikali kupitia Wizara ya Afya imeongeza fedha za kusomesha Wataalamu bingwa na bobezi hadi kufikia shilingi Bilioni 8 kutoka Shilingi Bilioni 3 za mwaka wa fedha 2021/22, utakaosaidia kuboresha huduma kwa wananchi na kupunguza Rufaa za nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Oktoba 28, 2022 wakati akitoa taarifa kuhusu mpango wa Serikali wa kuendeleza Watumishi wa Sekta ya Afya katika fani za ubingwa na ubingwa bobezi nchini mpango huo umepewa jina la Mpango wa Samia wa kuongeza wataalamu bingwa na bobezi wa afya nchini (Samia Health Super Specialisation Programme in Tanzania)

"Kwa mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imeongeza fedha za kusomesha Wataalamu bingwa na bobezi hadi kufikia shilingi Bilioni 8 kutoka Shilingi Bilioni 3 za mwaka wa fedha 2021/22 utakaosaidia kuboresha huduma za afya nchini. " Amesema Waziri Ummy.

Ameendelea kusema kuwa, ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa na bobezi nchini kuanzia mwaka huu wa fedha, Wizara imeanzisha mkakati mpya wa kutoa ufadhili kwa watumishi wa Sekta ya Afya kwa utaratibu wa set.

Utaratibu huu umeanzishwa ili kuhakikisha huduma za kibingwa zinazotolewa zinakuwa na wataalamu wote wanaohitajika ili huduma husika iweze kutolewa kwa ukamilifu, amesisitiza.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa, Wataalamu watakaosomeshwa kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu ya figo kikamilifu katika set ni kama ifuatavyo; Daktari Bingwa wa Upasuaji Figo, Daktari Bingwa wa matibabu ya Figo, Daktari Bingwa wa utoaji dawa ya Usingizi kwa wagonjwa wa Figo.

Daktari Bingwa wa Mionzi, Muuguzi Bingwa wa Mionzi, Mteknolojia Mionzi, Muuguzi Bingwa wa Figo, Muuguzi Bingwa wa Usimamizi wa huduma za chumba cha upasuaji kwa wagonjwa wa Figo na Mtaalamu wa Vifaa Tiba vinavyotumika kwa ajili ya matibabu ya figo, aliendelea.

Pia, Waziri Ummy amesema, jumla ya watumishi 139 wamechaguliwa kupata ufadhili wa masomo ambapo kati ya hao 136 watasomeshwa nje ya nchi na watatu (3) ndani ya nchi, ambapo Wizara itatoa ufadhili wa mafunzo ya set yaliyowasilishwa na Taasisi mbalimbali.

Sambamba na kufadhili watumishi 139 kwa utaratibu wa set pia watumishi 318 watafadhiliwa kwa utaratibu wa mtu mmoja mmoja na kufanya jumla ya watumishi watakaofadhiliwa kuwa 457 kwa mwaka wa fedha 2022/23, ambapo 146 (32%) ni wanawake. Kati ya watumishi 457 watakaofadhiliwa, 157 (34%) watasoma kwenye Taasisi za nje ya nchi.

 Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kukubali kuongeza fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 8 zitakazotumika kugharamia wataalamu waliochaguliwa kusoma mafunzo haya

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUITWA KWEYE USAILI WAOMBAJI NAFASI ZA AJIRA MTENDAJI WA KIJIJI III NA DEREVA II September 21, 2024
  • TANGAZO LA HALMASHAURI KUKUSANYA USHURU WA USAFI May 07, 2024
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA PROGRAM YA BBT May 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA DEREVA July 12, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAJALIWA AFUNGUA TAWI LA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR MKOA WA MOROGORO

    July 17, 2024
  • GAIRO SEKONDARI YATEKELEZA AGIZO LA KULIMA BUSTANI ZA MBOGAMBOGA, MATUNDA

    July 15, 2024
  • MARUFUKU KUUZA, KUNUNUA MAZAO KWA KUPIMA KWENYE NDOO, MADEBE

    July 12, 2024
  • KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI

    July 11, 2024
  • Tazama zote

Video

WANAFUNZI DARASA LA SABA WAASWA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni za Manunuzi
  • Zabuni za Ujenzi
  • Huduma

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Tanzania
  • GAIRO ONLINE TV
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Mawasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.

    Sanduku la Posta: 40, GAIRO

    Simu ya Mezani: +255 787730665

    Simu ya Kiganjani: +255 717222572

    Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa