Na. Cosmas Njingo, GAIRO
JANUARI 18.2023
Shirika la Maendelo lisilo la Kiserikali CRESD kupitia mradi wa kuwezesha AKINA MAMA WADOGO, limejikita katika kusaidia upatikani wa mitaji rahisi ili kuamsha upya ndoto za mabinti chini ya umri wa miaka 18, waliopata ujauzito na kujifungua, hali iliwasababisha kukatisha masomo na kushindwa kufikia ndoto zao.
Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Jackson Mahenge amesema CRESD inalenga kuibua miradi ya kusaidia vikundi vya Wamam Wadogo kujikita katika shughuli za uzalishaji na kiuchumi ili waweze kukidhi mahitaji yao ya kila siku sambamba na kuhudumia watoto wao.
Kwa kuanzia CRESD imepiga kambi Wilayani Gairo ikiwa ni mkakati wa kutekeleza malengo yake kwa vitendo, ambapo inatarajia kuwafiki Wamama Wadogo wapatao 80 kuwasaidia kupata mitaji na vifaa kwa ajili ya mradi wa ufugaji kuku kupitia vikundi.
Naye Meneja wa Mradi huo Wilayani Gairo Bi.Judith Mshigwa, alisema, kupitia shirika hilo la CRESD Wamama Wadogo watajengewa uwezo wa mbinu mbalimbali na elimu ya ufugaji bora wakuku, kuwapa mtaji wa vifaranga 150 kwa kila kikundi pamoja na vifaa muhimu vya kuendeshea mradi huo.
"Tutawapa vifaranga 150 kwa kila kikundi, lakini pia lazima tuwajengee uwezo wapate ujuzi na elimu ya ufugaji bora pamoja na kuwawezesha katika ujenzi wa mabanda bora ya kufugia". Aliseme Meneja huyo.
Februari 17.2023 Shirika la CRESD lilitambulisha na kuzindua rasmi mradi huo Wilayabi Gairo, ambao unalenga kurejesha matumaini mapya na kuongeza chachu ya katika kuwezesha kufikia ndoto za Wamama Wadogo ambao ambao ndoto zao zilikatishwa kutokana na sambabu mbalimbali ikiwepo Ndoa za Utotoni, Mimba zisizo tarajiwa na vitendo vya Unyanyasaji wa Kijinsia vilivyo sababisha kukatisha malengo yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa