Kaimu katibu Tawala (W) Bi. Annamarry Mwasendwa akifungua kikao cha Elimu ya Afya ya Msingi Julai 21.2022, kujadili hali ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele (Matende, Mabusha na Usubi) kwa ajili ya maandalizi ya kampeni ya ugawaji wa dawa za kuzuia maambukizi ya magonjwa hayo.
Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Serikali kwa kushirkiana na Wadau mbalimbali inaendelea kuhakikisaha inaimarisha mifumo ya utoaji huduma za afya ili Wananchi wake wapate huduma bora zinazoendana na Sera na Miongozo inayotolewa na Wizara.
Kauli hiyo imetolea na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame, katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi. Annamarry Mwasendwa wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili taarifa ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Julai 21.2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
“Serikali kwa kushirkiana na Wadau mbalimbali inaendelea kuhakikisaha huduma za afya zinaimarika ili kuwawezesha Wananchi wake kupata huduma bora za afya zinazo endana na Sera na Miongozo”. Alisema Bi. Annamarry.
PICHA 2: Mfumbo wa maumbile ya mwanaume unavyo athiriwa na ugonjwa wa MABUSHA/NGIRI MAJI
Alisema Maendeleao ya Watanzania yanaletwa na Wananchi wenye afya bora na imara, wenye uwezo wa kuzalisha mali, ambao wamejihakikishia usalama wa afya zao kutokana na uhakika wa upatikanaji wa huduma bora katika vituo vya kutolea huduma za afya Nchini.
Alifafanua kuwa, magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yanaendelea kuwa tishio zaidi katika maeneo ya unda wa Pwani, ambapo watu wengi hususani Wanaume wanapata magonjwa hayo lakini hawafanyi juhudu yoyote kutafuta tiba, na kwamba tamwimu zinaonyesha zaidi ya watu takribani milioni mbili wapo katika hatari ya kuambukizwa magonjwa hayo.
“Tafiti zinaonyeka kuwa Watu waishio katika ukanda wa Pwani wapo katika hatari ya kuambukizwa magonjwa hayo kwa zaidi ya silimi 45, hivyo lazima na sisi Wananchi wa Mkoa wa Morogoro tuchukue hatua za kujikinga na magonjwa hayo maana tupo jiarani na mikoa ya ukanda huu, ikiwepo Tanga na Mkoa wa Pwani wenyewe, hasa maeneo ya Bagamoyo”, alibainisha Kaimu Afisa Tawala huyo.
PICHA 3: Ugonjwa wa matende unavyo athiri sehemu za siri za mwanaume
Bi. Annamarry alitaja magonjwa hayo kuwa ni pamoja na Mabusha, Matende na Usumbu ambayo yanawakumba wanaume wengi nchini ingawa serikali inaendelea kufanya juhudi mbali mbali za kuhakikisha inatoa huduma za afya zenye kukidhi mahitaji wa wangojwa wenye matatizo hayo kwa kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi.
“Serikali yetu inapambana usiku na mchana kuimarisha mifumo yote ya utoaji huduma za afya, ikiwepo uhakika wa upatikanaji wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi, lengo ni kuona kunakuwepo na Tiba sahihiili kwa watu wenye magonjwa yasiyopewa kipaumbele”. Alieleza Bi. Mwasendwa.
PICHA 4: Ugonjwa wa Matende unaathiri miguu
Naye Dkt. Hizza Abdallah Hizza (mtaalamu wa magonjwa ya macho) akiwasilisha taarifa ya Magonjwa ya Mabusha, Matende na Usubi, kwa niaba ya Kaimu Mganga Mkuu (W) Dkt. Reuben Mfugale, alisema magojwa hayo yanatibika endapo wahanga watawahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mapema kabla tatizo halijawa kubwa.
PICHA 5: Dakta Abdallah Hizza akiwasilisha taarifa ya hali ya maambukizi ya magojwa yaliyokuwa ahayapewi kipaumbele
“Endapo mwathirika atwahi kwenda kupata huduma za afya kwenye vituo vya kutolea huduma, anajihakikishia uhakika wa kupona kabisa, lakini kitu kingine upo uwezekano wa kujikinga kuambukizwa kwa kumeza Dawa Kinga ambazo tunarajia kuanza kuzigawa hivi karibuni kupitia kampeni maalumu ya kutokomeza maambuzi ya Mabusha, Matende na Usubi”. Dkt. Hizza Alisema.
Dkt Hizza aliwaeleza wajumbe wa kikao hicho kwamba, Matende ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa viungo vya mwili hasa miguu na viungo vya uzazi ambao husababishwa na vimelea aina ya minyoo (parasitic worms) wanao enezwa na mbu jike aina ya culex na mbu dume jamii fulani ya (anopheles spicies).
Alisema “mbu hawa hueneza ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine
baada ya kumuuma mtu mwenye maambukizi na kubeba vimelea vya ugonjwa huu, na anapomuuma mtu asiye na maambukizi humuachia vimelea ambavyo huingia katika mfumo wa damu na kupitia hatua mbalimbali na kuanza kuzaliana hadi kuziba mfumo wa upitishaji wa maji mwilini”.
PICHA 6: Inzi Mweusi anayesababisha ugonjwa wa USUBI
Hizza alifafanua zaidi na kusema kuwa, minyoo hiyo huishi kwa miaka 4-6 kwenye mwili wa Binadamu, na katika uhai wake huzaliana mamilioni ya mabuu mengine wakati ikiwa kwenye mfumo wa damu.
Alisema mdhara ya ugonjwa huu ni kupoteza viungo, ulemevu wa kudumu na kuwa tegemezi, ambapo alitaja njia za kutibu ugonjwa wa matende ni pamoja na uvaaji wa viatu ni ili kujikinga kupata vidonda, Kusafisha eneo lenye uvimbe ili kuzuia wadudu, kutumia dawa kinga ambazo ni Evermectin, Albendazole, mabendazole.
PICHA 7: Mbu aina ya CULEX anaye eneza ugonjwa wa MABUSHA/NGURI MAJI
Ili kuepuka maambukizi ya Ugonjwa wa Matende Dkt. Hizza alisema ni muhimu Kuteketeza mazalia ya mbu (usafi wa mazingira), Kutumia vyandarua kwa usahihi.
Kuhusu MABUSHA Daktari huyo alisema ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa korodani za mwanaume ambayo hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani, inaweza tokea kwenye korodani moja au zote mbili kwa pamoja na kwamba zinaweza kuwatokea Wanawake kwa mara chache.
Aidha kwa upande mwingine alisema ugonjwa wa USUBI ni ugonjwa wa vimelea unaosababishwa na minyoo iitwayo onchocerca volvulus. Ugonjwa huu unasababisha ngozi kuwasha na ngozi kuwa na mabaka mithili ya mamba au mjusi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa