Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Japhari Kubecha, ameendelea na ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi ambapo Septemba 9, 2025 alitembelea Kata ya Idibo. Katika ziara hiyo, alikagua jengo la polisi linalotumiwa kwa muda na Jeshi la Magereza pamoja na mradi wa vyoo katika Shule ya Msingi Idibo. Ameahidi kuwa kufikia mwezi Desemba mwaka huu, kituo cha polisi cha Idibo kitazinduliwa na kuwa kituo cha kwanza cha kata katika wilaya ya Gairo, huku ujenzi wa vyoo shuleni humo ukikamilika ndani ya wiki mbili zijazo.
Aidha, Kubecha aliwasikiliza wananchi wa Idibo na vijiji vyake kuhusu changamoto za maji, umeme, na huduma za afya. Alielekeza Meneja wa Ruwasa kuhakikisha changamoto ya maji inatatuliwa ndani ya wiki moja, huku umeme katika vitongoji vitano ukitarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka. Kuhusu huduma za afya, alibainisha kuwa Idibo imepangwa kupata kituo cha afya ndani ya mwaka huu wa fedha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa