Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabir Omary Makame amewataka viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), na watendaji wa Serikali kushirikiana na Ofisi yake katika kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya chama tawala ili kuwaletea maendeleo Wananchi badalaya kuendekeza marumbani na majungu yasiyo na tija kwa Jamii.
Alisema hayo Juni 21 alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama za Mapinduzi Wilaya ya Gairo kwenya ofisi za Chama hicho alipofika kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogor Mhe. Martine Shigela kufuatia uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
“Sisi sote tunajenga nyumba moja hivyo hatuna sababu ya kugombania fito, tukumbuke lengo letu ni moja tu la kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi la kuwaletea maendelo Wananchi kwa kuhakikisha tunatimiza matarajio yao”, alisema Mhe. Makame.
Alifafanua kuwa msingi wa maendeleo ya Taifa lolote unajengwa katika dhana ya umoja, msikamano, ushurikiano na mahusiano mazuri baina ya viongozi ambao ni watekelezaji wa Sera mbalimbali pamoja na wananchi wenyewe ambao ni wanifaika wa fursa zamaendelo zinazo letwa na serikali kupitia miradi mbalimbali.
“Wananchi wana matarajio na imani kubwa sana kwa Serikali yao katika kuwaletea maendeleo kiuchumi na huduma bora za jamii, hivyo ni lazima sisi viongozi wa juu tushikamane kwa kuzungumza lugha moja kutumia muda mwingi kutafuta njia bora za kutatua kero zao badala ya kila kiongozi kuzungumza lugha yake tofauti na mwenzake”, alitanabahisha.
DC Makame aliahidi kutoa ushirikino wa kutosha kwa uongozi wa CCM Wilaya, sambamba na kuhakikisha ajenda kuu ya kuwahudumia Wana Gairo kwa kusikiliza na kutatua kero zao ili kuwaletea maendeleo anaitekeleza kwa nguvu zake zote kwa kutumia weledi na taaluma aliyonayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Willaya Mhe. Shabani Sajilo aliezea kufurahishwa kwake na ujio wa Mkuu huo wa Wilaya ya Gairo Mhe. Makame na kueleza kuwa Chama Cha Mapinduzi kipi tayari kumpa ushirikiano katika kushughulikia kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Sajilo alifafanua kuwa Wananchi wa Gairo ni wachapa kazi na wanabidii ya kujituma katika kuchapa kazi ili kujikwamua kiuchumi lakini changamoto zao hazitatuliwi kwa wakati na viongozi wa Serikali kutokana na marumbano ya mara kwa mara baina ya viongozi hao hali ambayo alisema inakwamisha juhudi za wananchi kujikwamua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa