Na Cosmas Njingo-GAIRO DC
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame amewataka askari wa kikosi cha usalama barabarani Wilayani humo, kuacha mara moja tabia ya kukamata kwa mabavu waendesha pikipiki za abiashara ya abiria maarufu Bodoboda, nabadala yake askari hao wawe vinara wa kusimamia na kufuata sharia.
DC Makame ametoa katazo hilo Julai 19/2021 kwenye kikao maalum na vijana waendesha bodaboda kutoka kata mbalimbali Wilayani Gairo alipokutana nao katika ukumbi wa Diana kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero zao.
Mhe. JOM alimwagiza Kamanda wa Polisi Wilayani Gairo kuhakikisha Askari wote wa usalama barabarani wanafuata na kuzingatia sheria za ukamataji wa makosa yanayotokana na uvunjaji wa sheria za usalama barabarini, sambamba na kuwatendea haki wanaowakamata ikiwepo kuwapa elimu ili kupunguza kasoro za kiutendaji zinazofanywa na Askari hao wakati wakitekeleza majukumu yao.
“Naagiza kuanzia sasa Askari wote wa usalama barabara wahakikishe wao wanakuwa vinara katika kusimamia sheria za usalama barabarana na kuzifuata badala ya wao kuwa mbele katika kusababisha kuongezeka kwa wimbi la makosa ya usalama barabarani”. Alionya.
Alisema kuwa swala la Askari wa Jeshi la Polisi kutumia mabavu katika oparesheni mbalimbali za kukamata wanao kiuka sheria za usalama barabarani, nao wanaji ingiza katika ukiukwaji wa sheria hivyo ni wajibu wao kutumia busara na hekima, sambamba na kujikita zaidi katika utoaji wa elimu ya usalama barabarani.
“Ni vizuri mkatumia nguvu nyingi kwenye kutoa elimu kwa hawa vijana wa bodaboda kuliko nguvu mnayotumia kuwakamata na kuwapiga adhabu za faini zisizo na tija kwao, lakini pia wengine mnawachukulia pikipiki zao na kuziweka kituoni kwa muda mrefu kwa makosa madogo madogo ambayo mngeweza kuyamaliza kwa utaratibu mzuri kabla ya kufikishana kutuo cha Polisi”, alieleza.
Aidha alimwagiza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabrani Wilayani humo kuhakikisha Askari wa Jeshi hilo wanavaa sare muda wote wanapo tekeleza majukumu yao ya kusimamia sheria za usalama barabarani ili kupunguza wizi wa pikipiki uliokithiri kutokana na baadhi ya Askari kusimamisha waendesha pikipiki bila kuwa kwenye sare hali ambayo alibainisha kuwa baadhi ya watu wanatumia mbinu hiyo kuiba pikipiki kwa kujifanya ni askari kumbe ni wezi.
Awali badhi ya waendesha bodaboda hao walimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwepo usumbufu wa askari wa usalama barabarabi kuwakamata bila kuvaa sare wawapo kenye shughuli za usafirishaji wa abiria na kwamba baadhi ya watu wanatumia mbinu ya kujivika kofia ya uaskari wakiwakamata na kudai kuwa pikipiki inapelekwa kituoni lakini wakifika kituoni hawazikuti pikipiki zao.
“Mhe Mkuu wa Wilaya kwa kweli tunapata shida sana na hawa Askari, wanatukamata bila sare na sisi tunasimama kuwaheshimu maana usipo simama ni kutengeneza tatizo zaidi, lakini bahati mbaya hata wezi nao wamegundua hilo, utakuta mtu anakusimamisha na kujitambulisha ni askari yupo kwenye opereshe maalum, unamuachia pikipiki kwa madai anaipeleka kituo cha Polisi ukiamini ni askari kumbe ni mwizi tu”, alieleza mmoja wa vijana hao.
Boda boda hao wakaongeza kuwa wanasikitishwa zaidi na wizi wa wa baadhi ya vipuri kwenye pikipiki pamoja na mafuta unaofanywa na Askari hao pindi pikipiki zao zikikamatwa na kushikiliwa kituo cha Polisi na kwamba wanapata wasi wasi na tabia ya baadhi ya askari kutokuwa wilizi wa mali za watu kwa kuwa nao kuingia kwenye matukio ya kihali ikiwepo wizi wa mafuta.
Naye mwakilishi wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Wilayani Gairo akijibu tuhuma hizo alisema amepokea malalamiko yao pampja na maagizo ya Mkuu wa Wilaya na kwamba atayafikisha kwenye uongozi wa juu wa Jeshi hilo kwa ajili ya utekelezaji ili kuhakikisha kero za boda boda hao zzinatatulika kwa njia ya kirafiki zaidi kwa lengo l akujenga mahusiano mazuri na vijana hao na kuimarisha polisi jamii ulizi shirikishi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa