Mkuu wa Wilaya ya Gairo ametoa vifaa vya ujenzi vyenye thaman ya shilingi zaidi ya Shilingi milioni mbili ikiwepo mifuko 118 ya sementi na bati 28 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule za msingi na sekondari, zahanati pamojaa na ofisi mbili za kata.
Akitoa salamu za Serikali kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa za robo ya tatu kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2021, kilichofanyika Juni 10 2021, kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Mhe. Mchembe alisema ofisi yake inatambua kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa ofisi za watendaji wa kata sambamba na upungufu wa vyumba vya madarasa shule za msingi na sekondari Wilayani humo.
“Mheshimiwa Mwenyekiti wa kikao hiki, ninapenda kulifahamisha Baraza lako la Madiwani kuwa, ofisi yangu pamoja na Kuu Wilaya tumetoa mifuko ya simenti na bati ikiwa ni juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu ya Afya na elimu kweye Wilaya yetu, ni matumaini yangu kuwa vifaa hivi vitatumika vyema kwenye kusaidia ujenzi wa madarasa katika baadhi ya shule zetu za Msingi na Sekondari”, alifafanua.
Miongoni mwa shule zilizonufaika na msaada wa mifuko ya sementini ni pamoja na Sekondari ya Chakwale ambayo imepata mifuko 10, Chigela Sekondari nayo imepewa mifuko 10, huku sekondari ya Mkalama imepewa jumla ya bati 28 kwa ajli ya chumba kimoja cha darasa.
“Waheshimiwa madiwani, Shule ya sekondari Gairo nayo ni miongoni mwa wanufaika wa vifaa hivi vya ujenzi, meipatia mifuko 10 ya sementi pamoja na Rubeho Sekondari nayo imapata itapata mifuko 10”, ali bainisha.
Shule nyingine za msingi zilizopewa mifuko ya sementi ni pamoja na Mkobwe B mifuko 16, Nongwe mifuko 16 na Rubeho mifuko 10.
Sambamba na shule hizo pia ofisi ya Mkuu wa wilaya Gairo imetoa jumla ya mifuko 30 ya sementi kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za watendaji wa kata ili kuwawezesha watendaji hao kufanya kazi kwa uhuru, amani na faragha pamoja na kuboresha huduma kwa wananchi usalama nyaraka mbali mbali za serikai.
Mhe. Mchembe alisema kata nyingi zina ukosefu wa ofisi za watendaji hali ambayo alitaja kuwa ni hatari kwa usalama wa Watendaji wenyewe na nyaraka wanazotumia kutekeleza maamuzi mbalimbali kwa kuwa wengi wao wanatumia nyumba zao za makazi kama ofisi za serikali hivyo ni vyema wakajengewa ofisi maalum kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao vizuri.
“Siyo salama hata kidogo kwa mtendaji wa kata kuendesha shughuli za Serikali nyumbani kwake hasa wakatai wa kutatua migogoro ya kijamii ikiwepo migogoro ya aridhi, mifugo na maswala ya kifamilia, kwa hiyo wanahitaji ofisi zinazo jitegemea ili wawe salama zaidi pamoja na kutunza nyaraka za serikali mahali salama”.
Alizitaja kata zitakazo nufaika na ujenzi wa ofisi za watendaji kuwa ni Iyogwe na Madege ambazo zimepata mifuko 10 ya sementi kila moja huku wananchi wa Kijiji cha Mogohigwa kata ya Chigela wakinufaika kwa mifuko 10 ya sementi itakayotumika katika mradi wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho.
Akiongea kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani wote, Mwenyekiti wa Halmasahauri ya Wilaya ya Gairo, Mhe. Rahel Nyangasi alimpongeza na kumshukuru Mkuu wa Wilaya Mhe. Mchembe kwa kuonyesha njia kama kongozi na kwamba waheshimiwa Madiwani watahakikisha wanasimamia vyema msaada alioutoa ili ukatumike kama ulivyoelekezwa katika maeneo yote.
“Kwa hili Mhemishimiwa Mkuu wa Wilaya nina kupongeza sana pia nachukua fursa hii kutoa shukrani zetu kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani wote hasa wale ambao kata zao ndiyo wanufaika wakubwa wa miradi uliyo weka nguvu zako”.
Aidha Mhe. Nyangasi aliwasihi madiwani wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wa juu wa Serikali Kuu pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea Wananchi maendeleo.
Kikao hicho cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kilipitia na kujadili hoja mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za maendelo katika robo ya tatu kwa kipindi cha Januari- Machi, ambapo pamoja na mambo mengine kiliwarejeshwa kazini watumishi wane wa Idara ya ujenzi waliokuwa wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kushindwa kusimamia vyema ujenzi wa Mabweni ya wasichana Shule ya Sekondari Gairo na Iyogwe, pamoja na kuwafutia mashitaka Maafisa watatu wa Idara ya elimu msingi waliokuwa wakishutumiwa kwa wizi wa mitihani ya Taifa wa Darasa la saba 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa