Na Cosmas M. Njingo GAIRO.
April 17
Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa shule za sekondari Wilayani Gairo, wametakiwa kufanya kazi kwa bidii, weledi wa hali ya juu, sambamba na kusimamia kwa waaminifu fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili utakelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo.
Rai hiyo imetolewa Aprili 17.2023 na Bi. Msifwaki Haule, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wakati akifungua Mafunzo ya ya siku moja ya Upimaji wa Vishiria Muhimu vya Kiutendaji kwa Viongozi hao, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
"Naomba niwakumbushe kuwa, sasa hivi Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Wito wangu kwenu, nendenei mkaisimamie kwa uaminifu miradi hiyo na kuhakikisha matumizi ya fedha yanaendana na uhalisia wa miradi hiyo". Alisema Bi. Haule.
Naye Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasimali watu Bw. Emmanuel Vulli, amawataka viongozi hao kufanya kazi kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za utumishi wa Umma ili kujiepusha kutenda makosa mbalimbali yatakayo sababisha kuchukuliwa hatua ikiwepo kufukuzwa kazi.
Kwa upande wake Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Gairo, Mwl. Juma Eustace, amewaambia walimu hao kuwa wanatakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa kwenye jamii kwa katika kuonyesha nidhamu na uadilifu
Awali kabla ya kuwasilisha mada ya Upimaji wa Viashiria Muhimu vya Utendaji, Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Mwl. Petronilla Wakurila aliwaasa watumishi hao kujiepusha na tabia ya kusambaza barua na nayaraka mbalimbali za Serikali kwenye mitandao ya kijamii hususani makundi ya whatsapp.
"Acheni mara moja tabia ya kutumiana nyaraka za Serikali kwenye Mitandao ya Kijamii. Barua nyingi zinatembea kwenye makundi yenu ya Whatsapp. Hii haikubaliki na nikosa Kisheria". Alionya Mwl. Wakurila
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa