Na. Cosmas Mathias Njingo
GAIRO, MOROGORO
Oktoba 30.2022
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imesema katika mwaka wa fedha uzajo 2023/2024 Wilaya ya Gairo itaingizwa kwenye mpango wa bajeti wa kutekeleza kilimo cha umwagiliaji ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia Nchi.
Naibu Waziri wa Kilimi Mhe. Anthony Peter Mavunde (MB) akihutubia Wananchi wa Kata ya Rubeho wakati akifunga maadhimisho ya Wiki la Kilimo Wilayani Gairo
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Anthony Peter Mavunde (MB) wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki la Mkulima liliohitimishwa katika kata ya Rubeho Wilayani Gairo Oktoba 29.2022.
“Wiki ijayo nitamuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Umwagiliaji aje hapa kuangalia hayo mabwawa ili mwaka ujao wa fedha 2023/2024 Wilaya ya Gairo tuingize kwenye mpango wa Bajeti ianze kutekeleza kilimo cha umwagiliaji”. Alieleza Mhe. Mavunde.
Naibu Waziri wa Kilimi Mhe. Anthony Peter Mavunde (MB) akihutubia Wananchi wa Kata ya Rubeho wakati akifunga maadhimisho ya Wiki la Kilimo Wilayani Gairo
Mavunde alisema serikali inaendelea kuweka juhudi mbalimbali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia Nchi, ikiwepo kuwekeza katika miradi ya umwagiliaji ili kuwawezesha wakulima kutoathiriwa na hali ya ukosefu wa mvua na kutegemea mvua za asili peke hali ambayo alisema inapunguza tija katika uzalishaji.
“Serikali inatambua hali ya mabadiliko ya Tabia Nchi, ndiyo maana wataalam wetu watakuja kufanya upembuzi yakinifu na kutoa mapendekezo yatakayosaidia Wizara kutenga bajeti ya uchimbaji mabwawa mapya na kufukua mabwawa yaliyopo, pamoja na kuweka miundombinu muhimu kwa ajili ya kuwezesha Wakuliam wengi zaidi wa Gairo kushiriki kweye kilimo cha umwagiliaji pasipo kutegemea mvua za misimu”. Alibainisha Naibu Waziri Mavunde.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mavinde (kulia) akikabidhi mbolea ya ruzuku kwa mmoja wa wakulima aliyetimiza vigezo na masharti vya kunufaika na mbolea za ruzuku zenye pumgulo la bei ya sh.60,000 kwa mfuko mmoja wa Kilogram 50, wakati wa hitimisho la wiki la Kilimo Kata ya Rubeho Wilaya ya Gairo.
Mavunde akaongeza kuwa Bajeti ya Wizara ya kilimo imeongezeka kutoka Shilingi Bil.294 mwaka 2021/2022 na kufikia kiasi cha shilingi Bil.954 kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Ongezeko ambalo alisema halijawahi kutokea tangia kupatikana kwa uhuru wa Tanzania Bara.
“Ongezeko hili halijawahi kutokea tangu enzi za kupigania Uhuru wa Tanzania Bara mwaka 1961. Wizara ya Kilimo haijawahi kupoikea fedha nyingi kama ambavyo imepokea katika mwaka wa fedha 2023. Hii ndiyo dhamira ya Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan”. Aliongeza Mhe. Mavunde.
Baadhi ya viongozi Waandamizi ngazi ya Wilya wakiwa na Mhe. Anthony Mavunde wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki la Mkulima kata ya Rubeho
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe.Jabiri Omari Makame akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mhe. Anthon Mavunde, kufunga Kilele cha Maadhimisho ya Wiki la Kilimo, alisema kupitia Wiki la Mkulima, zaidi ya Wananchi laki moja walishiriki katika maadhimisho ya wiki hilo na kwamba Wakulima na Wananchi wengi wamepata manufaa kutokana na elimu waliyopata kutoka kwa wadau mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri J. Makakme
“Zaidi wa Wanachi laki moja wameshirikik katika maonesho haya ya Wiki la Kilimo Gairo, ambapo tulitenga viruo vitatu ikiwepo kituo cha Ukwamani Gairo Mjini, Kituo cha Chakwa;e na Kituo cha Rubeho. Mhe Naibu Waziri kupitia Wiki hili lakilimo” alisema
Akaongeza kwamba “Wananchi na wakulima wamepata manufaa mbalimbali ikiwepo Elimu ya kanuni bora za Kilimo, wamepata Mbegu kutoka kwa mawakala wa mbegu waliopo katika viwanja hivi pamoja na mbolea za ruzuku ambazo Serikali imetoa Nchi nzima”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa