Na. Cosmas M. Njingo. Gairo Morogoro
Agosti.24.2022
Wilaya ya Gairo imepata heshima ya kuwa Mwenyeji katika mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 kimkoa, ambapo mwenge huo umepokelewa Agosti 24.2022 ukitokea Mkoani Dodoma na kukimbizwa Kiwilaya kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
(Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (Kulia)Mhe. Fatuma Mwasa, akiwa na Matibu Tawala wa Mkoa Dkt. Mussa Ali Mussa, wakati wa mapokezi ya mwenge wa Uhuru 2022 Kimkoa, Wilayani Gairo)
Akikabidhi Mwenye wa Uhuru 2022 na Wakimbiza Mwenge 6, kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatuma Mwassa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alisema, ukiwa Mkoani Dodoma Mwenge wa Uhuru 2022, Umekimbizwa umbali wa Km 132, umetembelea, na kukagua Miradi 39 yenye thamani ya Sh 14,156, 0000. Pamoja na kutangaza ujumbe wa Mwenge, sambamba na kuhamasisha Wananchi kujitokeza kuhesebiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Agosti 2022.
“Mimi Rosemary Senyamule, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ninakukabidhi Mwenge wa Uhuru 2022 ukiwa salama, unang’ara na unameremeta Mhe. Fatuma Mwassa, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Ninakukabidhi wakimbiza Mwenge 6 wa Uhuru Kitaifa, wakiongozwa na Kijana mahiri Sahiri Nyanzabala. Na ninakuombea kwa Mwenyezi Mungu”. Alisema Mhe. Senyamula.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatuma Mwasa akipokea Mwenge huo wa Uhuru 2022 pamoja na Vijana 6 wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa kutoka kwa Mhe. Senyamula, alisema; Ukiwa Mkoani Morogoro Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa umbali wa kilometa takribani 2,048,kuona, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 50, yenye thamani ya Sh.13.5 Bilioni.
(Wahe. Wabunge wa Mkoa wa Morogoro wakishiriki mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 Kimkoa, Wilayani Gairo Agosti 24,2022)
“Ninakiri kupokea Mwenge wa Uhuru ukiwa unang’ara na unameremeta. Aidha nakiri kupokwa Wakimbiza Mwenge 6 Kitaifa wakiongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 Kitaifa Makamanda wetu Jasiri, Shupavu na Mahiri Sahiri Geraluma”. Alisemma
Na kuongeza “Ukiwa Mkoani Morogoro Mwenge wa Uhuru Unatajiwa kukimbizwa umbali wa kilometa takribani 2, 048,kuonam kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 50, yenye thamani ya Sh.13.5 Bilioni. Nikuahidi kwamba Morogoro tupo timamu, tutaulinda, tutautunza na tutaukimbiza Mwenge wa Uhuru kwa Ujasiri na ueledi mkubwa”. Alitamba Mhe. Mwasa.
(Mwenge wa uhuru 2022 baada ya kuwasili Wilaya ya Gairo ukitokea Mkoani Dodoma)
Awali Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Sahili Geraluma Nyanzabala, alizitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatekeleza agizo la Serikali la kutenga 10% za mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya kuwezesha kiuchumi Vikundi vya uzalishaji mali vya Wanawake,Vinaja na Watu wenye Ulemavu.
(Wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2022, wakiongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Nd. Sahili (wapili kushoto)
“Ndugu zangu Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kote Nchini, Serikali imeagiza kila Halmashauri ihakikishe inatenga 10% kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya kiuchumi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu”. Alisisitiza Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Mabadi yaliyoa andaliwa kwa ajili ya utengenezaji wa Majiko katika mradi wa Vijana Kwawalesha kata ya Ukwamani)
Aidha Mwenge wa Uhuru 2022, ukiwa Wilayani Gairo utakimbizwa katika Tarafa ya Gairo, kwenye vijiji 11 kati ya 50 ambapo utapita kwenye miradi 6, kuona kuzindua na kuweka mawe ya Msingi. Miradi hiyo inatajwa kuwa na thamani ya Sh.Bilioni 1,198,476,916.72.
Mhe. Jabiri Omari Makame alitaja Miradi itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2022 ni pamoja na Mradi wa Vijana watengeneza Majiko katika Kitongoji cha Kwawalesha, Kata ya Ukwamani wenye thamani ya Sh 21, 439,680, kati ya hizo Sh. 15,000,000 zilizotokana na 4% sehemu ya Mkopo wa 10% kwa Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.
(Baadhi ya majiko yanayotengenezwa katika kiwanda kidogo cha Vijana watengeneza majiko)
Utazindua Mradi wa ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa shule ya Sekondari Majembwe, wenye thamani ya Tsh.78, 312,830.72, Utaweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharula (EMD) wenye thamani ya Tsh.259, 184,378.00.
(Mradi wa ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa Dharula, Hospitali ya Wilaya ya Gairo)
Miradi mingine itakayo wekewa Mawe ya msingi ni Mradi wa ujenzi wa Barabara ya Ramashop-Msingisi (Barabara ya Manyara) iliyojengwa kwa kiwango cha Lami wenye thamani ya sh. 247,637,790.00 fedha za Tozo ya miamala ya simu, na Mradi wa Kituo cha kuuzia mafuta (MC Petro Station), wenye thamani ya Sh.318, 000,000.
Pia Mwenge wa Uhuru 2022 utaweka Jiwe la Msingi katika Upanuzi wa Mradi wa Maji Makuyu kwenda Kinyolisi na Iyogwe, wenye thamani ya sh. 288, 336, 896.95, kisha utafuatiwa na Mkesha wa Mwenge wa Uhuru kwenye Viwanja vya Gairo ‘A’ shule ya Msingi, ambapo Agosti 25, Mwenge wa Uhuru 2022, utakabidhiwa Wilaya ya Kilosa.
(Mradi wa vyumba 4 vya madarsa shule ya sekondari Majembwe)
(Kuweka jiwe la msingi barabra ya Ramashio-Msingisi Guest (Barabara ya Manyara)
(Upanuzi wa Mradi wa Maji Kinyolisi, Makuyu hadi Iyogwe)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa