Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Halmashauri ya Wilaya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro imeendelea kufanya vizuri katika kusimamia matumizi ya fedha za umma kwa vipindi vinne mfululizo kwenye utekelezaji wa bajeti kuanzia mwaka wa fedha 2019/2020 hadi 2021/2022 na kupata hati ya kurudhisha kwa mujibu wa Hoja za Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG.
(Mhe. Martine Shugela, Mkuu wa Mkoa wa Morogor akitoa maelekezo kwenye kikao cha baraza maalum la Waheshimiwa Madiwani kujali hoja za Mkagunzi Mkuu na Mdhibiti wa fedha za Umma Juni 18/2022.)
Akitoa salam za Ofisi yake, Mkaguzi na Mdhibi wa Hesabu za Serikali (CAG) Mkoa wa Morogoro, Juni 17, 2022 kwenye Kikao cha Baraza Maalum la Madiwa kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri mjini Gairo, alisema Halmashauri zote tisa (9) za Mkoa wa Morogoro ikiwepo Gairo zimekuwa zikifanya vizuri katika kusimamia matumizi ya Fedha za Umma.
"Mhe. Mwenyekiti, nipende kuchukua fursa hii kulipongeza Baraza lako tukufu kwa kazi nzuri inayofanya katika kusimamia kikamilifu matumizi ya fedha za Umma hasa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Hii imeleta tija kwa Wananchi kwani miradi inaonekana jinsi inavyo wanufaisha, lakini kikubwa zaidi ni kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ni miongoni mwa Halmashauri tisa (9) za Mkoa wetu wa Morogoro zinazofanya vizuri kwenye eneo hili na zilizopata Hati ya Kuridhisha kwa kipindi cha miaka 4 mfululizo". Alibainisha CAG.
(Waheshimiwa Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Gairo katika kikao cha Baraza maalum la waheshimiwa Madiwani kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa hesabu za Umma (CAG)
Alisema kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ya Gairo ilipata jumla ya hoja za ukaguzi 14 kati ya hizo hoja nane (8) sawa na asilimia themanini na nane (88%) zilipata majibu na kufungwa huku hoja 6 sawa na asilimia kumi na mbili (12%) zikiendelea kutafutiwa majibu. Mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya hoja zilikuwa thelathini na nne (34), kati ya hizo ishirini na tisa (29) sawa na aslimia themanini na saba (87%) zimejibiwa na kufungwa ambapo hoja tano (5) sawa na asilimia kumi na tatu (13%) zinaendelea kutafutiwa majibu.
"Mhe. Mwenyekiti mwaka wa fedha 2019/2020 na 2020/2021 jumla ya hoja arobaini na nane (48) zilihojiwa na ofisi yangu, kati ya hizo hoja thelathini na saba (37) zilijibiwa na kufutwa kabisa, zipo hoja kumi na moja (11) hizi zinaendelea kuhama mwaka hadi mwaka kwani bado hazijapata majibu ya kuziondoa katika kuhojiwa", Alifafanua CAG.
CAG alifafanua zaidi kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ilihojiwa jumla ya Hoja 25, huku Hoja kumi na tatu (13) zikipatiwa majibu na kufungwa, wakati hoja kumi na mbili (12) zilizo salia bado zinaendelea kusubiri majibu ili ziweze kuondolewa.
"Mhe. Mwenyekiti, katika bajeti tunayo endelea kuitekeleza ya mwaka wa fedha 2021/2022 ziliibuka jumla ya Hoja ishirini na tano (25), lakini hadi sasa tayari hoja kumi na tatu 13 tumesha ziondoa baada ya kupatikana majibu yake, zimesalia Hoja kumi na mbili tu za ukaguzi ambazo tunaamini Menejimenti ya Halmashauri inaendelea kutafuta majibu yake ili nazo ikiwezekana tuzifunge kabisa". Alisisitiza.
Pichani (kushoto) Mhe. Rachel Myangasi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo (kulia) Mhe. Clement Msulwa, makama mwenyekiyi wa Halmashauri
Kwa upande mwingine CAG aliwataka Waheshimiwa Madiwani hao pamoja na Wataalam wa Halmashauri kuongeza nguvu katika kukusanya mapato kwa kipindi kilichosalia kukamilisha mwaka wa fedha 2021/2022 kuelekea mwaka mpya wa fedha 2022/2023 ili kufikia malengo ya makusanyo iliyojiwekea sambamba na kuendelea kusimamia kikamilifu matumizi yake.
"Niwaombe Waheshimiwa Madiwani na Wataalam wote kwa ujumla kuongeze nguvu na juhudi katika makusanyo ya mapato ya Halmashauri ili lile lengo mlijiwekwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 lifikiwe kuelekea mwaka mpya wa fedha 2022/2023. Muitumie vyema neema ya Mgodi wa Madini ya Dhahabu kule Kitaita". Aliongeza.
Mkutano huo wa Baraza Maalum la Waheshimiwa Madiwani kujadili Hoja za Mkaguzi Mkuu wa Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ulihudhuriwa na Mhe. Martine Shigela Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Mariam Ntuguja. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo Ndugu Shabani Sajilo, Katibu wa CCM Wilaya Bi. Highnes Munisi, Mhe. Jabiri Omari Makame Mkuu wa Wilaya ya Gairo,Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Viongozi wa Dini na Wenyeviti wa Vyama pendwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa