Halmashauri ya Wilaya Gairo imezindua rasmi zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali, ambapo iimeelezwa zaidi ya wafanya biashara 300 wamejisajiri katika mfumo maalumu wa vitambulisho huku idadi ikitarajiwa kuongezeka zaidi kufikiwa Juni 2021
Mhe. Siriel Shaidi Mchembe, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, amezindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa kugawa zaidi ya vitambulish0 200 kwa wafanya biashara wa soko la Msasani ambalo hufanyika jumanne ya kila wiki, huku akiwataka wafanya biashara hao kuvitumia vitambulisho hivyo kwa manufaa ya kujikwamua kiuchumi kupitia biashara ndogo ndogo wanazofanya ili kuiwezesha serikali kuwa na mfumo mzuri wa ukusanyaji mapato.
Amesema vitambulisho hivyo vikitumika vizuri vitawasaidia wajasiliamali hao kupata mikopo inayotolewa na Halmashauri katika mgawanyo wa asilimia 10 ambapo hutolewa kwa wanawake asilimia 4, vijana asilimia 4 na walemavu 2 na kwmaba hiyo itawawezesha kujiongezea mitaji na kukuza biashara zao.
“Vitambulisho hivi vimekamilika kabisa, maana vimebeba taarifa muhimu za mjasiriamali husika, hivyo mvitumie vizuri vitawasaidia katika kupata mikopo itakayo wawezesha kuongeza mitaji na kukuza biashara zenu, lakini pia nia ya serikali yetu ni kuwa na mfumo mzuri, bora na imara wa kukusanya kodi”.
Aidha amewataka wafanya biashara ndogo ndogo maarufu kama wajasiriamali kuhakikisha wote wanakata vitambulisho vya ujasiriamali ili waweze kufanya biashara zao kwa uhuru na amani pasipo kubughudhiwa na mamlaka zinazohusika na utozaji ushuru, ambapo amesema ulipaji wa ushuru kwa kila siku ni gharama kubwa ikilinganishwa na kukata kitambulisho kinacho gharimu shilingi elfu ishirini tu kwa mwaka.
Akizungumza wakati akipokea vitambulisho kwa niaba ya wafanya biashara wengine Makamu Mwenyekiti wa Soko la Msasani Hamiss Hassan, amesema upatikanaji wa vitambulisho hivyo umeondoa kero ya kulipa ushuru wa shilingi elfu mbili kwa siku ambapo amebainisha kwa mwaka inafikia shili laki tano na ishirini elfu, na badala yake vitambulisho hivyo vimeokoa kiasi cha shilingi laki tano kwa malipo ya shilingi elfu ishirini tu kwa mwaka mzima.
@C.M. Njingo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa