Na. Cosmas Mathias Njigo. GAIRO DC.
Uchambuzi umeonesha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imeongoza katika uhabarishaji Wananchi Kitaifa kwa asilimia 89 ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa 87 na Halmashauri ya Wilaya ya Muheza asilimia 83.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. InnocentBashungwa (MB) kuhusu mapato na matumizi ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/22 iliyo tolewa Jijini Dodoma Agosti 2.2022.
Taarifa hiyo ilisema upimaji huo unalega kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinatekeleza kwa vitendo dhana ya Uwazi, uwajibakaji na Utawala bora katika kufikisha taarifa sahihi kwa Wananchi kuhusu pesa zinazotolewa na Serikali za utekelezaji wa Miradi mbaimbali ya Kimaendeleo kwa Jamii.
“Moja ya wajibu wa Halmashauri ni kuhakikisha fedha zinazopelekwa kwa Wananchi katika maeneo yao pamoja na miradi inayotekelezwa inafahamika kwa Wananchi ili waweze kufuatilia na kusimamia matumizi sahihi ya fedha hizo”, Ilisema sehemu ya Taarifa hiyo ya Mhe. Bashungwa.
Taarifa hiyo ikaeleza zaidi kuwa Sehemu ya utoaji mrejesho na uhabarishaji Umma imeonesha namna ambavyo Halmashauri ziliweza kuwajibika na kuongeza uwazi kwa Wananchi kwa kuwahabarisha juu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali ikiwemo Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.
Taarifa imeonesha jinsi Halmashauri zilizovyoweza kutumia vema tovuti zao kwa kuweka taarifa muhimu na kuhuisha kila taarifa zinavyopatikana. Katika eneo hili kwa kuanzia uchambuzi umefanyika kuangalia maeneo ya tarehe ya mwisho kuweka taarifa kwenye tovuti, uwepo kwa taarifa za viongozi wapya, idadi ya taarifa (Mei na Juni) na uwepo wa taarifa za bajeti za Halmashauri zilizoidhinishwa na Bunge.
kuhusu tahmini ya hali ya ukusaji mapato kwa mwaka wa fedha 2021/2022, taarifa hiyo imeainisha ufanisi wa kila Halmashauri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kulinganisha makisio yaliyoidhinishwa na hali halisi ya utekelezaji.
Aidha, taarifa hii imeonesha pia namna Halmashauri zilivyotekeleza vigezo vingine ambavyo vimeonekana ni muhimu pia vikafanyiwa tathmini kwa lengo la kuongeza uwajibikaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
“Hivyo, taarifa hii imejumuisha sehemu mbili, sehemu ya kwanza ikiwa ni ufanisi katika ukusanyaji wa mapato,matumizi ya makusanyo hayo ya ndani katika shughuli mbalimbali za kuwaletea Wananchi maendeleo ikiwemo matumizi ya mapato katika Miradi ya maendeleo, usimamizi wa mikopo ya asilimia kumi inayotokana na mapato ya ndani”, Alisema Mhe. Bashungwa kupitia taarifa hiyo
Kwa upande mwingie pia taarifa hiyo iliainisha namna ambavyo halmashauri zilijibu hoja na kutekeleza mapendekezo ya CAG na namna Halmashauri zinavyoimarisha utawala bora kwa kuhabarisha umma juu ya shughuli mbalimbali zinatekelezwa na Serikali. Sehemu ya pili imetoa taarifa ya tathmini katika vigezo vyote kwa kutoa alama kulingana na uzito wa kila kigezo na jinsi ambavyo Halmashauri imefikia alama za jumla.
Katika mwaka wa fedha 2021/22, Halmashauri zilipanga kukusanya Shilingi Bilioni 863.9 kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani. Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Juni 2022, Halmashauri zimekusanya Shilingi Bilioni 888.7 ambayo ni asilimia 103 ya makisio ya mwaka.
Uchambuzi wa taarifa za mapato ya ndani ya Halmashauri katika mwaka wa fedha 2021/22 unaonesha kuwepo kwa ongezeko la mapato halisi yaliyokusanywa kwa kiasi cha Shilingi bilioni 131.7 ikilinganishwa na kiasi halisi kilichokusanywa katika mwaka wa fedha 2020/21 cha Shilingi Bilioni 757.1 sawa na ongezeko la asilimia 17.
Kiwango hicho hakijawahi kufikiwa kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita kwani Halmashauri hazijawahi kufikia malengo yao ya mwaka kwa asilimia 100
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa