Serikali imetenga kiasi cha shilingi 84.7 Bilioni kwa ajili ya kukamilisha mradi wa usambazaji umeme katika vijiji vyote vya Mkoa wa Morogoro, ambapo Wilaya ya Gairo peke yake imepewa jumla ya Shilingi Bilioni 3 kutekeleza mradi huo kwa kipindi cha miezi 18.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dakta Medardi Kalemani amezindua mpango wa utepelekaji umeme vijijini awamu ya tatu na kwamba Vijiji vyote 50 vya Gairo vitanufaika na mpango wa utekelezaji wa kusambaza umeme vijijini REA huku kipaumbele kikielekezwa katika vijiji vilivyopo Tarafa ya Nongwe.
Dakta Kalemani alisema kwamba Gairo imekuwa Wilaya pekee kwa Mkoa wa Morogoro kuwa mwenyeji wa uzinduzi rasmi wa utekelezaji wa Mpango huo, na kuongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imrdhamiria kujenga na kuboresha uchumi wa Watanzania wenye kipato cha chini kwani kupitia miradi huo wakulia watweza kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo.
“Kwa niaba ya Wana Gairo ninamshukuru sana Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwani ametoa pesa za kutosha kukamilisha upesambazaji umeme katika vijiji vyote vya Wilaya ya Gairo, kwa hiyo swala la kuunganisha umeme majumbani sio la hiari tena ni la lazima, lakini pia Serikali yetu imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 1.024 katika kutekeleza Mradi wa REA nchi nzima”, alibainisha.
Akimkaribisha Waziri Kalemani, Mkuu wa Mkoawa Morogoro Mhe. Martine Shigela aliwambia Wananchi kuwa upatikani wa umeme huo utaongeza ya thamani ya mazao ya wakulima kwani kutarahisisha usindikaji wa mazao hayo kwa kujenga viwanda vidogo vidogo vijijini na kupata soko kwa urahisi sambamba na kuongeza ajira.
“Mradi huu ni mkombozi Mkubwa sana kwa wana Gairo hususani wakazi wa vijiji vilivyopo Tarafa ya Nongwe, kilichopo sasa ni kuwa wabunifu kufikiria namna ya kuongeza thamani ya mazao yenu kwa kujenga viwanda vitakavyo wezesha kufanya usindikaji rahisi wa mazao, lakini pia kuzalisha ajira kwa vijana wenu”, alisema Waziri Dakta Kalemani.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe. Ahmed Shabbiby alimwambia Waziri Kalemani kuwa Tanesco Wilayani humo wanafanya kazi nzuri usiku na mchana lakini wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Gari kwa ajili ya ufuatiliaji, kufanya ukaguzi katika maeneo yenye miundo mbinu mibovu pamoja na huduma ya dharula pale panapotokea kukatika umeme.
“Mhe. Waziri kwa kweli Meneje wa Tanesco anafanya kazi nzuri sana nampongeza, ila ombi langu kwako ni moja tu, umpatie gari ili kumrahisishia kufanya ufuatiliaji na matengenezo ya dharula pale panapo tokea kukatika umeme”, Alisema Mhe. Mbunge.
Aidha Waziri Dakta Kalemani aliahidi kutoa gari aina ya Land Cruiser pickup kama ilivyo ombwa na Mbunge Mhe. Shabbiby ambapo alimwagiza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme (Tanesco) kuhakikisha Gari hilo linafikishwa Ofisi za Tanesco Gairo kufikia juma tano ya wiki ijayo.
Hafla hiyo ya uzinduzi wa Mradi wa usambaji umeme vijijini Kimkoa ilifanyika Juni 17 kwenye kijiji cha Mheza Ititu Kata ya Rubeho Wilayani Gairo, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwepo, Mheshimiwa Martine Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Waheshimiwa wa Kuu wa Wilaya za Mkoa wa Morogoro, Wabunge wa majimbo ya Gairo, Kilosa, Mikumi na Mvomero, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Mwenyekiti wa Halmashauri Bi. Rahel Nyangasi, Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Agness Mkandya pamoja na viongozi waandamizi wa kampuni zilizopewa kandarasi ya mradi huo na wanachi kutoka vitongoji vya kijiji cha Kisitwi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa