• Mawasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
GAIRO DISTRICT COUNCIL
GAIRO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Authorities Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira
    • Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni za Halmashauri
      • Seksheni ya Rasilimali Watu
      • Seksheni ya Utawala
    • Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Baraza la Madiwani
  • Miradi
    • Miradi ya Maendeleo
      • Sekta ya Elimu Msingi
        • Miradi Mipya
        • Miradi iliyokamilika
      • Sekta ya Elimu Sekondari
      • Sekta ya Afya
      • Sekta ya Barabara/Miundombinu
      • Sekta ya Maji
  • Machapisho
    • Katiba ya JMT
    • Sheria ndogo ndogo za Halmashauri
    • Hotuba Mbalimbali
    • Sera ya Elimu
    • Taarifa za Hesabu za Mwisho
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

GAIRO YAZINDUA MASHINDANO YA KOMBE LA SENSA

Posted on: August 16th, 2022


Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame amezindua mashindano ya Mprira wa Miguu kuwania Kombe la Sensa (Gairo Sensa Cup) lengo ikiwa nikuendeleza zoezi la hamasa na utoaji wa elimu kwa Wananchi wa Wilaya hiyo kupata uelewa wa pamoja ili washiriki kuhesabuwa ifikapo Agosti 23.2022.

(Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame (mwenye miwani) akiongoza matembezi ya amani kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi Agosti 13.2022) 

Uzinduzi huo ulitanguliwa na maandamano ya matembezi ya amani yakiongozwa na Mhe. Makame, na kuitikiwa kwa ari kubwa na Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wananchi, Watumishi wa sekta za Umma na Binafsi, Wafanya Biashara pamoja na Wasanii mbalimbali waliojitokeza kushiriki katika kuhamsihsa Sensa ya Watu na Malazo.

Awali kabla ya uzinduzi huo wa Kombe la Sensa Gairo kwa michuano ya mpira wa miguu, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Makame alisema matembezo hayo ya amani ni ishara ya kuonyesha kwamba Wanagairo wapo tayari kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kuanza tarehe 23.08.2022.

(Viongozi wa Vyama vya Siasa wakishiriki kwenye uzinduzi wa Tamasha la Sensa na Michuano ya mpira wa Miguu ya Kombe la Sensa (Gairo Sencer Cup) Agosti 13.2022)

“Ndugu zangu matembezi haya ni ishara ya kuionyesha Tanzania nzima kuwa sisi Wananchi wa Gairo tumeamua kuwa kauli moja kwamba ifikapo tarehe 23 Agosti, sote tutajitokeza kuhesabiwa na tutatoa ushirikiano kwa makarani wa”. Alisema Mhe. Makame.

Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Jabiri Omari Makame akawataka Wananchi kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi kwa Makarani wa Sensa ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi zitakazo saidia kupanga mipango enedelevu kwa kuzingatia mahitaji ya Wananchi wake.

(Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya-Gairo All Stars wakitumbuiza katika uzinduzi wa Tamasha la Sensa, Agosti 13.2022)

“Kushiriki Sensa ni wajibu wa kila Mwananchi na kila Mtanzania atakaye lala nchini uskiku wa kuamkia tarehe 23 mwezi wa nane 2022. Kila mmoja awetu akitokeze kuhesabiwa na kuhakikisha taarifa zinazokusanywa ma karani wa sensa ni taarifa sahihi”. Alisema Mhe. Makame.

Mkuu huyu wa Wilaya akatumia fursa hiyo kuwaasa Makarani wa Sensa kuwa waaminifu, wakweli na wazelendo, pamoja na kujiepusha na vitendo vitakavyo hatarisha usalama wa taarifa watakazo zikusanya na maisha yao wenyewe huku akitolea mfanya wa Ngoswe aliyejitumbukiza kwenye mapenzi wakati wa sensa na kusahau majukumu yaliyokuwa mbele yake.

“Kuweni waangalifu, waaminifu na wakweli, lakini pia wajibu wenu ni kukusanya taarifa na siyo kwenda kujiingiza katika vitendo ambavyo vitahatarisha usalama wenu na taarifa mtakazo zikusanya. Tukumbuke habari ya Ngoswe kumpenda Mazoea Binti wa Mzee Ngengemkeni Mitomingi na kusahau kazi iliyompeleka pale, ninaimani sote tunajua nini kilitokea”. Aliwaasa.

(Baadhiya makari wa Sensa ya watu na Makazi wakishiriki kwenye uzinduzi wa tamasha la Sensa, Agosti 13 2022)

Kwa upande wao viongozi wa Vyama vya Siasa Wilaya ya Gairo walisema zoezi la sensa ni zoezi muhiomu kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa letu na kwamba ni muhimu kila Mwananchi kushiriki bila kujali itikadi za vyama vyao kwani maendeleo hayana chama.

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Gairo Bwn. Ernest Boniphace alisema chama chake kipo tayari kushirikiana na uongozi wa Wilaya kutoa elimu wa Wanachama wa chama hizo na kwa wananchi wengine kwa kuwa zoezi la Sensa ni zoezi muhimu kwa mustakabali wa Serikali kupanga mipango bora ya kuwafikiashia Wananchi wake Maendeleo bila kujali itikadi za vyama na kuongeza kuwa Maendeleo hayana Vyama.

“Sensa ya watu na Makazi ni zoezi muhimu sana kwa Taifa letu, kwani inaiwezesha Serikali yetu kujua idadi ya watu, mahali walipo, mahitaji yao, hali zao za ajira na kipato; ili iweze kupanga na kutoa huduma kwa kuzingatia takwimu zitakazo patikana baada ya Sensa. Ndiyo maana chama cha CHADEMA tumeamua kushiriki kwa nguvu zote kwenye tamasha hili ikiwa ni kuonyesha Umma wa Watanzania kuwa Sensa na Maendeleo havina Vyama bali ni fursa ambayo kila Mtanzania anastahili kuipata”. Alifafanua Bwn. Boniphace.

Naya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya, Bwn. Shabani Sajilo amewataka wenyeviti wa Vitongoji vya Mamlaka ya Mji mdogo pamoja na Wenyeviti wa vijiji kuhakikisha wanashirikiana na Watenda wa Kata na Vijiji kutoa elimu na kukamasisha Wananchi washiriki katika zoezi hili pamoja na kuhakikisha kaya zote zinafikiwa na makarani wa Sensa ili kupata takwimu sahihi.

(Mashabiki wa Timu ya Simba Wilaya ya Gairo nao hawakuwa nyuma kwenye hamasa la Sensa)

“Mimi wito wangu ni kwenu Wenyeviti wote wa vitongoji vya Mamlaka ya Mji Mdogo na Wenyeviti wa Vijiji, hili ni jambo lenu na niwajibu wenu kam viongozi kuhakikisha kaya zote zinafikiwa na Makarani wa Sensa na kila Mwananchi amehesabiwa. Mkashirikiane na Watendaji wa Kata na Vijiji katika kusimamia zoezi hili liweze kufanikiwa”. Alisisitiza Mwenyekiti huyo wa CCM Wilaya ya Gairo.

Uzinduzi wa kuwania Kombe la Sensa (Gairo Censor Cup) ulitanguliwa na mtanange mkali baina ya Timu ya Watanashati FC na Lushwaji FC, na kuchagizwa na Tamasha la Sensa likisheneni burudani kutoka kwa Wasanii wa Gairo All Stars pamoja na michezo mbalimbali ikiwepo kukimbiza Kuku, Kuvuta Kamba na mchezo mingine.

(Baadhi ya wanachi walioshiriki tamasha la Sensa gairo)

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUITWA KWEYE USAILI WAOMBAJI NAFASI ZA AJIRA MTENDAJI WA KIJIJI III NA DEREVA II September 21, 2024
  • TANGAZO LA HALMASHAURI KUKUSANYA USHURU WA USAFI May 07, 2024
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA PROGRAM YA BBT May 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA DEREVA July 12, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAJALIWA AFUNGUA TAWI LA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR MKOA WA MOROGORO

    July 17, 2024
  • GAIRO SEKONDARI YATEKELEZA AGIZO LA KULIMA BUSTANI ZA MBOGAMBOGA, MATUNDA

    July 15, 2024
  • MARUFUKU KUUZA, KUNUNUA MAZAO KWA KUPIMA KWENYE NDOO, MADEBE

    July 12, 2024
  • KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI

    July 11, 2024
  • Tazama zote

Video

WANAFUNZI DARASA LA SABA WAASWA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni za Manunuzi
  • Zabuni za Ujenzi
  • Huduma

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Tanzania
  • GAIRO ONLINE TV
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Mawasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.

    Sanduku la Posta: 40, GAIRO

    Simu ya Mezani: +255 787730665

    Simu ya Kiganjani: +255 717222572

    Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa