Na. Cosmas Njingo, GAIRO.
Sekta ya Afya Wilayani Gairo imeimarika na kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa Mama na watoto kiasi cha kupunguza vifo kutoka 13 mwaka 2021/2022, vifo 8 Mwaka 2022/2023, kufikia vifo 2 kuanzia Januari hadi Novemba 2023.
(Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Sharifa Babalanga'nya, akizungumza kwenye na Waandishi wa Habari wa Kampeni ya kuelezea Mafanikio ya Serikali kwa kipindi cha miaka 3 ya Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, uliofanyika Novemba 2.20223).
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Bi. Sharifa Nabalang'anya wakati akieleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita yaliyopatikana kupitia fedha za utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2012/2022 hadi 2023/2024; kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari wa Kampeni ya kuelezea Mafanikio ya Serikali kwa kipindi cha miaka 3 ya Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, uliofanyika Novemba 2.20223.
(Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Sharifa Babalanga'nya, akizungumza kwenye na Waandishi wa Habari wa Kampeni ya kuelezea Mafanikio ya Serikali kwa kipindi cha miaka 3 ya Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, uliofanyika Novemba 2.20223).
(Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Sharifa Babalanga'nya, akizungumza kwenye na Waandishi wa Habari wa Kampeni ya kuelezea Mafanikio ya Serikali kwa kipindi cha miaka 3 ya Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, uliofanyika Novemba 2.20223).
Alisema mafanikio ya Serikali inyoongozaa na Rais Dakta Samia Suluhu Hassan yanaonekani wazi kwani zaidi ya TSh. Bil 2 zimetumika kwenye ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa zahanati mpya 9 na vituko vya Afya 2.
(Baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro wakihudhuria kikao na Waandishi wa Habari wa Kampeni ya kuelezea Mafanikio ya Serikali kwa kipindi cha miaka 3 ya Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, uliofanyika Novemba 2.20223).
Kuhusu Sekta ya Elimu Msingi, Bi. Nabalang'anya alisema Halmashauri ilipokea fedha kiasi cha Tsh. 2.8 Bilioni za ujenzi wa Shule mpya mbili za Awali na Msingi, ujenzi wa vyumba vipya 39 vya madasara, umaliziaji wa vyumba 47 vya Madarasa,ujenzi wa Nyumba 5 (2/1) za Walimu na ujenzi wa matundu ya vyoo, ikiwa ni mkakati wa Serikali ya Mhe. Samia ya kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Sambamba na hayo pia Mkurugenzi huyo alisema Serikali ya Mama Samia imewasikia na kuwafikia Wananchi wa Gairo kwani kupitia fedha hizo, Halmashauri imekamilisha ujenzi wa Bweni la Wasichana Wenye uhitaji maalum katika Shule ya Msingi Ukwamani.
Mkurugenzi Nabalang'anya alisema Wananchi wa Gairo wanazo sababu za kumshukuru Mhe. Dakta Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa Shule Mpya 3 za Sekondari na maboresho ya miundombinu mbalimbali katika Shule za zamani, ambapo kiasi cha Tsh 3,800,000,000 zilitolewa kwa ajili ya miradi hiyo ya Elimu Sekondari.
Akizungumza Sekta ya Utawala alisema Serikali Kuu ilipeleka fedha katika Halmashauri hiyo TSh.485,000,000 kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi, pamoja na TSh za ujenzi wa 4 za Wakuu wa Divisheni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa