Na, Cosmas Mathias Njingo
GAIRO, Morogoro
Sepetemba 23.2022
Katika mwaka wa Fedha 2020/2021 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kupitia Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, dawati la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi ilitoa Mkopo wa Shilingi milioni 104, 771,000 kwa cikundi 14 vya wajasiliamali ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuhakikisha unawawezesha wananichi kiuchumi kupitia vikundi vya Wanawakem Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Kiasi hicho cha Fedha ni 10% ya Makusanyo ya mapato ya ndani, ambayo hurejeshwa kwa Wananchi kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa mitaji kwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa lengo la kupambana na umaskini kwa kuweka mazingira rafiki ya uwezeshaji kiuchumi.
Kwa mujibu wa Afisa Maendelea ya Jamii na Mkuu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi. Stella Simon Ngomano, Sehemu ya Mkopo wa 10% za mapato ya ndani ya Halmashauri imechanganuliwa kwa kuzingatia vigezo na maelekezo ya Serikali lengo ni kuhakikisha makundi yote yaliyokubalika yananufaika na mikopo hiyo.
Mchanganuo huo umeainisha kuwa asilimia nne (4%) inaelekezwa kwa Vikundi vya Wanawake, asilimia nne (4%) kuwanufaisha vijana na asilimia mbili (2%) ni kwa ajili ya makundi ya Watu wenye Ulemavu.
Bi. Stella Ngomano anabainisha kuwa, kwa mwaka 2020/2021 jumla ya Vikundi tisa (9) vya Wanawake vilinufaika na mkopo wenye thamani ya Shilingi 43,361,000 milioni, Vijana Vikundi 2 vilikopeshwa jumla ya Shilingi 44,300,000, huku Jumla ya Shilingi 17,110,000 zilitoletolewa kwa Vikundi vitatu (3) vya Watu wenye Ulemavu.
“Fedha hizi za Mkopo wa 10% zilitolewa kwa jumla ya Vikundi 14, kati ya hivyo, Wanawake Vikundi 9 vilikopeshwa mkopo wenye thamani ya milioni 43,361,000 fedha za kitanzania, Vijana Vikundi 2, vilikopeshwa milioni 44, 300,000, Watu wenye ulemavu Vikundi 2 vilikopeshwa kiasi cha Shilingi 17,110,000 milioni. Mkopo huo ni kwa mwaka wa Fedha 2020/2021”. Alifafanua Bi. Ngomano, Mkuu wa Dawati la Uwezeshaji Kiuchumi.
Kwa kutambua umuhimu wa kupambana na umaskini kwa Watanzania, mnamo mwaka 2004 Serikali ikatoa mwongozo kupitia Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, kwa kuhakikisha inaweka mazingira rafiki kwa Wananchi wake, kupata mitaji kupitia mikopo isiyo na riba ili waweze kubuni na kuanzisha miradi ya uzalishaji mali itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kupata kipato cha kuendesha maisha yao.
Uwezeshaji huo pia unalenga kutatua changamoto za Ukosefu wa masoko ya uhakika au uwezo wa kuingia katika masoko yenye ushindani, Ukosefu wa ushirikiano, ushirika hafifu na ukosefu wa sauti ya pamoja ya makundi mbalimbali ya wananchi katika kusimamia maslahi yao, na kukabilina matatizo yanayowakwaza wasishiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi katika sekta mbalimbali.
Vikundi vya Wanawake vilivyowezeshwa kiuchumi na kupatiwa mkopo kwa mwaka wa Fedha 2020/2021 ni pamoja na Wanyenda (5,000,000), Uhuru (13,841,000), Milako (5,720,000), Wamama Tuungane (2,000,000), Chikikole B (2,540,000) pamoja na kikundi cha Jitegemee kutoka kijiji cha Mamvisi kata ya Chanjale (2,000,000).
Vikundi vingine ni Dorkas (7,000,000), Wasamalia (2,360,000) na kikundi cha Amani kutoka kijiji cha Ching’olwe kata ya Chanjale ambavyo vyote kwa pamoja vimepata mkopo wenye thamani ya Shilingi 43, 361,000 (milioni arobaini na tatu, laki tatu na elfu sitini na moja).
Kwa upande wa Vikundi vya Vijana ni pamoja na Rubeho Transportes (23,500,000), na kikundi cha Boda boda Ibuti (20,800,000), wakati Vikundi vya wenye ulemavu ni Faraja (5,500,000), Umoja wa Walemavu Gairo (8,550,000) na Uvumilivu (8,560,000).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa