Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kupitia Idara ya Afya imeanza kutoa huduma mpya ya Dawa Kinga ili kusaidia kupunguza ongezeko la maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa makundi mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa kudhibiti UKIMWI upande wa Afya Dakta Lightness Mtaita wa kituo cha Afya Gairo wakati wa kikao cha Kamati ya kudumu ya Kudhibiti UKIMWI ya Halmashauri kilichofanyika Julai 13.2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
(Wajumbe wa Kamati ya Kudhibiti Ukimwi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo)
“Mheshimiwa Mwenyekit na Wajumbe wa Kamati hii, ninapenda kuwajulisha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imeanza kutoa huduma ya Dawa Kinga kwa ajili ya kupunguza maambukizi ya Virus vya UKIMWI, hususani kwa makundi ambayo yanatajwa kuwa kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi”, Alisema Bi. Mtaita.
Alitaja makundi yaliyopo kwenye hatari ya kupata maambukiz ni pamoja na Wanawake wanaofanya biashara ya ngono maarufu kwa dada poa, mapenzi ya jinsi moja hasa wanaume kwa wanaume (Ushoga), Wenza wenye majibu tofauti baada ya kupimwa V.V.U, pamoja na watumiaji wa Dawa za Kulevya kwa kujinga.
“Dawa hizi zitatolewa kwa makundi lengwa ambayo nimeyataja hapo juu, maana tayari yanatambulika kwa kuwa washirika wa makundi hayo wengine nimepata bahati ya kukutana na kuzungumza nao ana kwa ana pamoja na kuwahudumia”. Alifafanua.
(Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo katika kikao cha Kamati ya Kudhibiti UKIMWI)
Alisema kuwa tabia ya mapenzi ya jinsi moja (ushoga) biashara ya ngono kwa wanawake (dada poa) na matumizi ya Dawa za Kulevya inaanzia ngazi ya familia na kwamba jamii inawatambua watu wa aina hiyo lakini bado haijukui hatua ya kukemea tabia hizo.
“Mheshimiwa Mwenyekiti wengine tunaishi nao kwenye jamii zetu, na tabia hizi zina anzia kwenye ngazi ya familia, hivyo ni wajibu wetu sote kuhakikisha tunashirikiana kupunguza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI katika jamii zetu hasa hasa kwa makundi haya ambayo ndiyo yapo kwenye hatari kubwa ya maambukizi ya IKIMWI”. Alieza.
Kwa upande mwingine Bi. Mtaita aliwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI kuwa zoezi la upimaji wa Virusi vya UKIMWI kwa hiari linaendelea kupitia utaratibu mpya wa Jipime Mwenye (Selftest) ambapo mteja atapewa maelekezo namna ya kutumia kifaa cha kupimia maambukizi hayo kwa njia ya majimaji katika kinywa.
(Mhe. Clement Msulwa (Diwani) Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI)
“Huduma ya kipimo cha Selftest itatolewa kwa wale wasiotaka kwenda kupimwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa kuogopa kujulikana hali zao za maambukizi ya V.V.U, hii inawagusa sana washirika wa ngono (sex partners) ambapo akibainika mmoja kuwa ameathirika atapewa maelekezo ili akawapime washirika wake kwa kutumia kipimo hiki”. Alifafanua Dakta Mtaita.
(Mratibu wa UKIMWI (w) Ndugu Mohamed Amri)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa