Huduma ya maji kwa wakazi wa vijiji vya Tabu Hoteli, Ngiloli, na Ibuti katika kata ya Chigela inatarajiwa kurejea kufuatia kukamilika kwa kazi ya kuchimba Kisima kipya cha maji kutokana na hitilafi ya pampu ya kisima cha awali kutumbukia kisimani.
Wakazi hao walikabiliwa na adha ya ukosefu wa maji baada ya kisimi walichokuwa wakikitegemea kupata huduma hiyo pampu yake kuzama kwenye kisima na kusababisha ugumu katika kuitoa.
tayari sasa Maji yamepatikana kazi inayofuata ni kuunganisha kwenye Mtandao Ili wakazi hao waweze kunufaika
Hii ndiyo maana halisi ya #Kaziiendelee. Hatimaye Wakazi wa Kata ya Chigela wataondokana na adha ya ukosefu wa maji iliyodumu kwa wiki moja kufuatia moja ya pampu katika kisima kilichokuwa kikizalisha maji eneo la ngiloli kupata hitilafu na kutumbukia kisimani, hali iliyosababisha Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuchimba kisima kingine ili kuwaondolea adha wakazi wa Vijiji vya Tabu Hoteli, Ngiloli, na Ibuti.
Julai 24.2023 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Makame alifika katika eneo hilo kujionea kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima hicho ambapo pia alishuhudia uzalishaji wa maji ambayo yataunganishwa kwenye mtandao wa Bomba la kusafirisha kwenda kwenye tangi tayari kusamabazi maji kwenye vituo na makazi ya watu.
Hongera Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan kwa kazi kubwa ya kuwaletea huduma Wana chigela
(Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame, akitazama hali ya uzalishaji wa maji baada ya kazi ya kuchimba kisima kipya kukamilika katika kijiji cha Ngiloli kata ya Chigela)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa