Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Hamlashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Susan Nyanda amewataka Wakuu wa Idara na vitengo na Maafisa bajeti wa kila idara kushirkiana na watendaji wengine katika idara zao kuandaa na kupanga kwa pamoja mpango wa bajeti inayotekelezeka sambamba na kuweka vipaumbele katika bajeti ijayo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Ametoa wito huo Disema.17.2021 wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya siku 2 juu ya Mfumo wa PlanRep iliyoboreshwa kwa ajili kuandaa mpango wa bajeti za idara mbalimbali za Halmashauri kuelekea upangaji wa bajeti mpya kwa mwaka wa fedha 2022/2023, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
“Mtumie fursa hii muhimu kujifunza kisha mkakae pamoja na watumishi wengine katika idara zenu ili muanda bajeti inayotekelezeka kwa kuzingatia mahitaji muhimu na kuweka vipaumbele vitakavyo tumika kwenye maandalizi ya bajeti mpya katika mwaka wa fedha ujao wa 2022/2023”, alielekeza Bi. Nyanda.
Kaimu Mkurugenzi Nyanda akatumia nafasi hiyo kuwaonya washiriki wa mafunzo hayo kuacha tabia ya kutoka toka kwenye chumba cha mafunzo, na badala yake wawe watulivu, waongeze usikivu na umakini pindi wawasilishaji wanapoelekeza hatua muhimu za kufuata katika mchakato wa kuandaa bajeti kupitia mfumo huo mpya wa PlanRep iliyoboreshwa.
“Nina wataka mtulie na muwe makini sana kwa kipindi chote cha mafunzo, punguzeni kutoka toka nje ili msipitwe na mwendelezo wa mada, nisingependa kusikia malalamiko kutoka kwa wazeshaji kuwa kuna hali ya utovu wa nidhamu au watu kutotulia kwenye chumba cha mafunzo”, alionya Kaimu Mkurugenzi Nyanda.
Naye mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo Bwana. Mussa Mshana aliwambia washiriki hao kuwa swala la kupanga bajeti na kusimamia utekelezaji wake siyo jambo la Afisa Mipango bali ni swala la idara husika moja kwa moja, hivyo ni vyema kila idara ikapanga bajeti kwa kuweka vipaumbele muhimimu vinavyotekelezeka ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza wakatai wa kutekeleza bajeti hiyo.
“Naomba nisisitize kuwa bajeti siyo ya Afisa Mipango wa Wilaya. Hapa ijulikane kuwa mmiliki mkuu na mtekelezaji namba moja wa bajeti ni Mkuu wa Idara husika na watumishi waliopo katika idara hiyo, hivyo niwajibu wenu kukaa pamoja kwenye idara zenu na kuweka vipaumbele vinavyokubalika na vinayotekelezeka”, alifafanua Bwn. Mshana.
Mafunzo hayo ya siku 2 yameanza Disemaba 17 na yatakamilika Disemba 18.2021, yanaedeshwa na Maafisa wawezesha kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikioa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa lengo la kuawjegea uwezo wakuu wa idara na vitengo pamoja na watumishi wengine kuwa na stadi muhimu za namna ya kuandaa bajeti kwa kuzingatia vipaumbele vya idara vinavyotekelezeka kuelekea kwenye maandalizi ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Miongoni mwa wawezeshaji wanaoendesha mafunzo hayo ni pamoja na Mchumi kutika OR-Tamisemi Bwana Adlrahiman Khatibu, Afisa TEHAMA Bi. Esther Mussa na Bwana Mussa Mshana, ambapo imeelezwa kuwa baada ya mafunzo hayo washiriki hao watakuwa na ujuzi na mbinu za kutosha kupanga bajeti yenye tija na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa